12 January 2016

KOCHA WA SIMBA KERR 'OUT' SIMBA

Na Sheila Ally
KOCHA mkuu wa Simba, Dylan Kerr ana asilimia kubwa ya kutimuliwa baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kitakachofanyika kesho asubuhi jijini Dar es Salaam ambapo kocha huyo atalazimika kufuta programu yake ya mazoezi ya asubuhi.


Habari za ndani kutoka Simba zinasema kuwa viongozi wa Simba hawajaridhishwa na kiwango cha timu yao kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ambalo wameshindwa kutetea ubingwa huo kwa kufungwa na Mtibwa Sugar jana katika hatua ya nusu fainali.

Chanzo hicho kimesema kuwa sababu nyingine ambayo imewaudhi viongozi wa Simba ni pale Kerr alipoamua kumtukana kocha wa Taifa Stars, Boniface Mkwassa baada ya kutoa ushauri juu ya kikosi chao kuwa kiongezewe mazoezi ya 'fitiness'.

Kikao hicho kitaamua kama kuvunja mkataba wake baada ya kumalizika kwa kikao hicho au kumpa muda mpaka baada ya mechi yao ya Ligi Kuu na Mtibwa Sugar itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Kuna kikao kesho ambapo Kerr anatakiwa kuja Dar es Salaam ni kikao ambacho kwa asilimia kuwa atafukuzwa. Kama si kesho hiyo hiyo basi ataambiwa mechi yake ya mwisho ni hiyo ya Jumamosi. Kerr anafahamu kinachoendelea juu yake hivyo anasubiri lolote litakalotokea," alisema kiongozi huyo

Kwa upande wa Mkwassa alisema: "Niliombwa ushuari na viongozi wa Simba ambao waliniuliza timu yao ina tatizo gani nikawashauri basi ndipo ilipotokea kupishana kauli na Kerr,".

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname