Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Simon Sirro.
Stori: Na Makongoro Oging’,
DAR ES SALAAM: Baadhi ya benki nchini zinadaiwa kuajiri baadhi ya wafanyakazi walio kwenye mtandao wa majambazi kutokana
na wateja wengi kupigwa risasi na kufa wakitoka kuchukua pesa,
uchunguzi wa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi Tanzania umebaini.
Hayo
yalisemwa na baadhi ya askari hao wiki iliyopita walipozungumza na
mwandishi wetu na kusema kwamba, waajiri wasipokuwa makini katika
kuajiri watashangaa kuona wateja wao wanapigwa risasi na kuuawa kila
kukicha.
“Haiwezekani
kuwa wanaonyang’anywa fedha ni wale wanaotoka kuchukua benki kuliko
wanaopeleka! Ina maana wezi wapo katika baadhi ya mabenki hivyo
kunatakiwa kuwepo na umakini wakati wa kuwaajiri,” alisema askari mmoja
kutoka makao makuu ya jeshi hilo, Dar akiomba hifadhi ya jina lake kwa
vile yeye si msemaji.
Afande
huyo aliendelea kusema kuwa, baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa
benki hizo wanapoona mteja anachukua fedha nyingi hufanya mawasiliano
kwa njia ya simu kuwaeleza majambazi walio nje namna alivyovaa mteja
huyo na kiasi cha fedha alichochukua.
Uchunguzi
zaidi unaonesha kuwa, endapo hali hiyo haitadhibitiwa haraka huenda
wananchi wakapatwa na hofu ya kuweka fedha zao benki kwa kuogopa kuporwa
na kupigwa risasi wakienda kuzichukua.
Uwazi
mwishoni mwa wiki iliyopita, lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam, DCP Simon Sirro (pichani) ambapo alikiri kuwepo kwa
baadhi ya wafanyakazi wenye mtandao na majambazi huku akisema jeshi lake
limeweka mikakati kuhakikisha mtandao huo unasambaratishwa mara moja.
“Ni
kweli kwamba, baadhi ya mabenki, si yote, yameajiri baadhi ya
wafanyakazi, si wote wenye mtandao na majambazi. Kwa hiyo hata wao ni
majambazi tu.
“Sasa
tumejipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kukamata pikipiki zinazohusika
katika uhalifu. Pia tumeamua kuweka makachero nje na ndani ya mabenki,
wapo polisi wa miguu, pikip iki na magari. Nina uhakika tutawadhibiti,”
alisema Kamanda Sirro.
Aliendelea
kusema kuwa, majambazi waliopo katika Kanda ya Dar es Salaam waanze
kufunga virago kwani bila kufanya hivyo wajue watakamatwa wote na
mtandao wao kumalizika. Pia aliwataka wamiliki wa mabenki kuwa makini
wakati wa kuajiri wafanyakazi ili kuwapata wenye sifa njema na kuweka
imani kwa wateja wao.
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman
Kova aliwahi kutamka kuwa, baadhi ya wafanyakazi wa ndani wa baadhi ya
benki wana ushirikiano na majambazi. Akawatahadharisha wamiliki kuwa
makini wakati wa kuajiri
No comments:
Post a Comment