Mbwana Samatta ndio jina liliotajwa zaidi kwenye vinywa vya
watanzania wengi na Afrika kiujumla ndani ya masaa kadhaa yaliyopita –
baada ya mwanasoka huyo wa Kitanzania anayekipiga katika klabu ya TP
Mazembe kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Anayecheza Ligi za
Ndani ya Afrika.
Ushindi wa Samatta, ambaye ni mshindi wa na mfungaji bora wa ligi ya
mabingwa wa Afrika umetokana na kuwashinda wapinzani wake Zein Edin
Farahat, Roger Assale, Robert Kidiaba, Moudather el Tahir,Mohammed
Meftah, Kermit Erasmus, Felipe Ovono, Baghdad Bournedjah, na Abdeladim
Khadrouf.
Utaratibu wa CAF – Shirikisho la soka katika upigaji kura wa
kumchagua mshindi wa tuzo hii unatokana na kura zilizopigwa na makocha
wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vya nchi za
kiafrika.
Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa hapo juu walipigiwa kura
na matokeo ni kama yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini.
Mbwana
Samatta alipata jumla ya kura 127 na hivyo kuongoza, akifuatiwa kwa
mbali na mchezaji mwenzie wa TP Mazembe Robert Kidiaba aliyepata kura 88
na aliyefunga Top 3 ni Baghdad Bournedjah. Kura zilipigwa na mataifa
45 ya nchi wanachama wa shirikisho la soka Afrika CAF.
Kwa upande wa Tuzo aliyoshinda Aubemayang kura zilikuwa hivi:
1- @Aubameyang7 143 points
2- @YayaToure 136 points
3- @AyewAndre 112 points
Mbwana Samatta pia alifanikiwa kutajwa katika kikosi bora cha Afrika cha mwaka 2015
No comments:
Post a Comment