Leo ni siku ya mazishi ya mzee Peter Abdallah Kisumo ambae ni mwasisi na
ameshika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwaziri, ukuu wa mikoa
na uenyekiti wa mashirika mbalimbali ya umma na mazishi yanatarajiwa
kufanyika kijijini kwao Usangi katika wilaya ya Mwanga katika makaburi
ya familia.
Kisumo aliaga dunia Agosti 3, 2015, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Dar es Salaam, ambako alikuwa anapatiwa matibabu ya figo, ikiwa ni
mwezi mmoja tangu arejee nchini akitokea nchini India.
Msafara wa Mhe.Lowassa wazuiliwa na wananchi mosh wakililia kumuona maeneo ya Boma akitokea KIA kuelekea msibani Mwanga..
Polisi wa Mwanga mkoani Kilimanjaro wamezuia msafara wa Edward Lowassa
kijiji cha Maroro Wilayani Mwanga sasa hivi akiwa ameongozana Mbatia,
Ndesamburo na Augustino Mrema ukielekea msibani kwa madai kuwa
wanaosindikiza msibani ni wengi sana.
No comments:
Post a Comment