09 July 2015

Zigo" Video ya AY imefanyika Tanzania, AY atoa sababu za kutofanyika nje ya Tanzania.


Tumekuwa na mazoea kuona video za wasanii wakubwa Tanzania kufanyika nje ya Tanzania, AY amepanga kuja na kitu tofauti baada ya kufanya video ya Zigo hapahapa Tanzania na kuwa kinyume na watu waliofikiria kuwa atafanya nyimbo hii nje ya nchi.


Akizungumza katika 255 ya XXL Ay atoa sababu za kuifanya video hii Tanzania chini ya Mtayarishaji Nisher. Ay amesema "Nilikuwa nataka nimpatie jukumu mtanzania mwenzangu, pili nataka tutumie location za Tanzania na ya tatu ni kwamba sipendi kufanya kitu ambacho kila mtu atategemea ntafanya kitu cha aina flani, let say mi nikisema nafanya video kwa mtu ambae anafikiria haraka haraka atasema naenda kufanya South Afrika kwa Godfather" alimaliza AY

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname