Natumaini mko poa,nilipokuwa kijana na balehe nilikuwa napenda sana
wasichana, yaani nilikuwa natamani sana wanawake wazuri wote wawe wangu,
siku mmoja niliposafiri kwenda kijijini kwetu, nikakutana na vijana wa
kule kijijini tulikuwa tunapiga story kuhusu mambo ya wasichana, ndipo
tukafikia hizo story za kutumia madawa kuwavutia wanawake ndipo kijana
mmoja akaniambia babu yake ana dawa nzuri sana ya hizo mambo.
Kwa vile kipindi kile nilikuwa napenda sana wasichana nilimwambia
anipeleke kwa babu yake nikachukue hiyo dawa, nilipofika kule
nikamwambia yule babu shida yangu ya kupata dawa ya mvuto kwa wasichana,
yule babu akaniambia ana dawa mbili ya kuoga na ya hirizi nichague ipi,
nikachagua ya hirizi, akaniambia natakiwa nimeze hiyo hirizi ndogo na
akanipa na dawa ya maji ninywe ikiwa imechanganywa na damu sijui ni ya
mnyama gani.
Baada ya kumeza hirizi na kunywa ile dawa ya maji, yule babu akaniambia
kuanzia siku hiyo hakuna mwanamke atakaye nikataa nikimtongoza. Sasa
imepita miaka kumi na moja, sijawahi kukataliwa na mwanamke yoyote
niliyemtongoza na nimeshakula pesa za wanawake wengi.
Sijawahi kumuomba hela mwanamke akaninyima labda asiwe nayo. Sasa hivi
juzi kati, dada yangu nae ameanza kunitongoza anadai anavutiwa na mimi
kimapenzi, anasema amevumilia sana ameshindwa imebidi aniambie, najaribu
kumuepuka lakini wapi.
Jamani hii dawa inanitesa sana, najuta kuitumia. Imenifikisha pabaya.
Naombeni ushauri wenu
No comments:
Post a Comment