Vanessa Mdee.
Maarufu
kama Vee money yeye ni recording artist, rapper, songwriter, na
mtangazaji wa vipindi vya television na redio,mitandao mengi ya huko
nchini Kenya ili ripotiwa kumfananisha mrembo huyu na mmoja wa
wanamuziki wa destiny child,Kelly Rowland.ndiye msanii anayetoka poa
kwenye kila aina ya vazi atakaloamua atupie,unaweza kudhani kuwa ni
model au kwa nini hajawa model nakuchagua kuwa muimbaji kwa jinsi alivyo
tu.
Najma.
Sauti
yake na uzuri wake kwa mara ya kwanza kuonekana katika luninga,ni
kwenye video ya tabasamu ya Mr.Blue,ila kutokana na uzuri wake,naamini
asilimia kubwa ya watu huishia kumuangalia Najma tu,naamini hata
asingekuwa na sauti nzuri watu bado wangekuwa wanaangalia video
zake,mbali na uzuri huo yeye pia ni msanii wa bongo fleva na kwa hivi
sasa ana-hit na track yake mpya ya Nimechoka aliyomshirikisha Aslay.
Meninah
Urembo
wake ulijionyesha pamoja na kipaji chake kizuri cha kuimba pale
alipoamua kushiriki mashindano ya Epic Bongo Star Search,ndio Tanzania
ilipoanza kuona uwepo wake,Shaghala baghala ndiye video yake iliyomuweka
kwenye ramani ya bongo fleva mwaka huu,nakufanikiwa kuzidi kupata
umaarufu,uzuri wake unaweza kusema labda amechovya flani hivi.
Jokate.
Ingawa
aliweza kuonekana kwenye nyimbo kadhaa za bongo fleva hapo mwanzo,
kupitia uzuri wake akiwa kama model,mwisho wa siku akajaribu kuweka
vocal,zikakubalika,nakushirikishwa kwenye nyimbo mbali mbali ikiwemo
kaka dada.Huyu si tu msanii wa bongo fleva,bali ni Tv presenter na host
katika events mbalimbali,ukiachia mbali u-CEO of Kidoti Lovig co.
Recho.
Wengi
humfananisha msanii huyu na mkongwe wa muziki wa Bongo fleva maarufu
kama RayC,kuanzia macho,weupe wake,sauti hadi jinsi anavyocheza unaweza
kusema kuwa ni mdogo wake Ray C,ila uzuri wake ndio uitakaokuweka kwenye
luninga yako muda mrefu kumwangalia video yake,badala yakusikiliza
nyimbo.Ni msanii aliyekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva nakukubalika
kirahisi na kubaki on top hadi hii leo,ana-hit na nyimbo kama
Kizunguzungu,upepo,nashukuru umerudi na nyingine nyingi.
Linah.
No comments:
Post a Comment