Ndoa
yangu sasa ina miaka 8, tuna watoto 3 na tumejenga nyumba mbili, wiki
mbili zilizopita mke wangu alibakwa na watu wawili waliokua wamejenga
nae ukaribu kwa lengo la kumhadaa. Siku ya tukio alipigiwa simu na hao
jamaa kwamba kuna shamba limepatikana Bagamoyo hivyo wakaliangalie
sikuwahi kujua kama anahitaji shamba.Ilikuwa ni Jumapili asubuhi
akaniacha home nimepumzika akaenda ili alione hilo shamba.
Hatukuwasiliana
tena hadi saa nne usiku nilipotaka kujua mwenzangu yuko wapi simu
iliita tu bila kupokelewa, nilishtuka kwa kweli maana hana tabia ya
kutonipokelea simu, baada ya muda ikawa haipatikani, nikaanza kumpigia
kwa namba yake ya Tigo ambayo iliita tu bila kupokelewa, ilipofika saa
sita usiku nikampigia mama yake mzazi nae anasema kwa siku hiyo hajafika
pale nyumbani.
Tukapeana
jukumu la kuendelea kumtafuta hewani ingawa sio mara ya kwanza kurudi
home mida hiyo, wakati mwingine anakuja mida hiyo anadai anatoka Kitchen
Party na kadi anakuwa nayo kweli, nikimuuliza kwanini hakuomba ruhusa
anajibu ""ningekuomba ungenikatalia"."
Hivyo
nikajipa moyo kuwa huenda ameenda kwenye Kitchen Party kama siku
zingine nikaendelea kusubiri, hadi saa nane usiku wapi hajaonekana, na
bahati mbaya hakwenda na Gari lake siku hiyo lilikuwa na matatizo kwenye
injini lilikuwa likisumbua wiki yote hiyo, nikaamua kwenda kwao usiku
huo huo, nikamwambia housegirl kuwa mama akija sipo mnipigie ila mkae
macho yenu yakiwa getini maana Leo hana Gari.
Tukiwa
kwao tayari ilikuwa saa Tisa usiku tukashauriana kwenda Muhimbili baada
ya kushauriwa na binamu wa wife aliepigiwa simu na mama mkwe usiku huo.
Kwa upande wa majeruhi hakuwepo, nikapelekwa walipozipanga maiti
zilizoingia usiku huo na ambazo hazijaenda mochwari sikufanikiwa, mama
mkwe aliogopa kuzitazama.
Saa
kumi na mbili asubuhi nikamrudisha mama mkwe kwake nami nikaa hapo hadi
saa tatu nilipoona simu ya wife ya Tigo ikiita nikapokea, ni sauti ya
kike ya mtu mwingine mwanamke. Kumbe wale jamaa wawili walimwekea dawa
za kulevya wife kwenye soda hivyo akazimika na kuchukua chumba Gesti na
kumwingiza humo, asubuhi tukaenda na ndugu kwa wife na mama mkwe baada
ya kupokea hiyo simu ya binti wa mapokezi ambae alitumia simu ya wife ya
kitochi waliyomwachia kitandani na kunipigia baada ya kukuta jina la
hubby.
Tulipofika
tulienda kwenye Chumba hicho tulikuta wife anakoroma na kutoa udenda
wenye damu kwa mbali, pembeni yake kulikuwa na kondomu zilizotumika na
kinyesi kiasi, mama yake alianza kulia kwa sauti.Kaka yake akampa kibano
kikali receptionist aseme ukweli lakini binti wa watu akasema hajui
chochote kuna watu wawili waliingia wamembeba na kulipia, na wakatoka
asubuhi na mapema.
Anyway,
kwa kifupi ni kwamba alitibiwa, alikaa hospital siku tano akipewa dripu
na dawa za kuondoa sumu mwilini, hadi hali yake ikawa sawa, kwa
ushirikiano alioutoa kwa polisi, na kwa kutumia TCRA ambao wana
wapelelezi wao wanaoshirikiana na CID madalali wale walikamatwa wote
wawili, mhudumu Wa gesti akaunganishwa kwenye kesi hiyo ya ubakaji
ingawa yeye mashtaka yake yanasomeka tofauti na wenzie.
Wamepandishwa
kizimbani mara moja na kesi yao kutajwa na imeahirishwa, wapo Segerea,
sijajua walishindwa masharti ya dhamana au nini kilitokea maana mimi
nilijitoa kwenye kesi hiyo nimewaacha ndugu waendelee nayo, nina sababu.
Tulikotoka na mwanamke huyu:-
Kiukweli
Haya yaliyompata ni matokeo ya kunidharau na kutoniheshimu kama mumewe,
amekuwa mtu wa ratiba masaa 24/7 per week, anachoamua anakifanya bila
consultation na Mimi, mfano:-Aliamua kujiunga na masomo ya jioni baada
ya kazi kama ifuatavyo. Alijiunga na diploma ya IT ucc inayoanza saa 11
jioni hadi saa moja jioni, hapo hapo akajiunga na masters ya MBA
inayoanza saa moja na kuisha saa nane usiku usiku hadi kufika home ni
saa tano na kitu nikamuuliza familia yako nani atai attend? Majukumu
yako nani atayafanya? Akanijibu ndio hivyo nimeshajiunga, hakuwa na
sababu ya kujiunga na IT angeanza na masters (prioritizing)
Wakuu,
mambo yake yote ni siri hasemi mipango yake, anajifanya mtu wa madili
anadili na wanaume kuhusu biashara mbali mbali bila kunishirikisha
ingawa ni muajiriwa. Mama yake ndio msiri wake mkubwa.
Akienda
kokote atoi taarifa hadi akifika huko ndio anasema "" hny nipo kwenye
send off"".Nikajaribu kutafuta huenda ana mwanaume nje lakini kiukweli
upepelezi na intelligence iliyotukuka ilithibitisha pasipo na shaka kuwa
hajawahi Ku cheat.
Simu
zake zote niliwahi kuziweka under 24 hrs surveillance kupitia watu
wangu wanaofanya kwenye mitando ya simu lakini mawasiliaƱo yote na
wanaume ni ya kikazi na madili mbalimbali. Pia niliwahi ku hack namba za
simu na account za kijamii zote pia nilitoka bila bila. Lakini hata
bedroom life ni nzuri tu, maana ukishindwa kumshika mke kwingineko basi
utamshika kwenye haki ya ndoa, mwanamke hawezi kutumikia wanaume wawili
kusionekane kasoro,lakini hata upande huo kwa kweli hakuna tatizo.
Sababu
niliyoigundua ni mali alizoachiwa na marehemu baba yake ambazo wamepewa
mirathi kama miaka minne iliyopita, wapo watatu, baba yao aliacha plot
na nyumba nyingi kwenye prime areas hivyo mke wangu amepewa sehemu
nyingi anazochukua kodi kubwa sana achilia mbali sehemu alizouza. Hivyo
ni mkakati wake na mama yake anifiche vitu vingi ili nisije kumdhulumu
anaona ni bora ashirikiane na mama yake kwenye mambo yake.
Hati
zangu anajua zilipo in case nimeanguka ghafla ila za kwake zote
alizopewa plot zaidi ya 6 ambazo tayari amebadilisha tayari majina kuja
ya kwake kazificha nisipopajua nimeshachoka, nashukuru Mungu hili tatizo
la kubakwa na kulawitiwa limetokea nimepata pa kumwachia, nasubiri awe
vizuri psychologically nianze mchakato wa talaka. Naomba muelewe sikuja
hapa kuomba ushauri bali kuwapa funzo wa akina dada na wengine.
Maana
nilimwambia hivi. """ hizi mbio zote unazokwenda resi ipo siku
watanipigia simu nikufuate Mochwari au Muhimbili"". Na kweli imetokea.
Sina haja na pesa zake nina zangu nazopata kazini nilizofanyia maendeleo
makubwa tu na miradi kadhaa.Wanashangaa kwanini sijihusishi na hiyo
kesi, ni kwa sababu nilimuonya mtoto kwao hakusikia na akanidharau,
tried to be a man and more than a man lakini ndo tunazidi kuvurugana.
Maana kuna watakaokimbilia kudai "" act like a man"" humu Jf as walikuwa
wanaona I am not acting like one.
Mungu
akikupa mke wa ovyo hata uki act like Tyson haitasaidia kitu. Sasahivi
wamerundikana hapo nyumbani mara leo wamletee pastor, kesho wamletee
counselor, mimi jioni naenda zangu kwenye bia narudi nipo vizuri
nalala.Juzi alikuja mshauri nasaha kuniambia ameniletea habari njema
vipimo vimeonesha wife hana HIV so natakiwa nifurahi.
Nikamjibu
mwambie afurahi mwenye matokeo mwenyewe mimi sitaendelea nae, sasa
sijui amewaambia, maana mama mkwe ananiangalia jicho kama vile
anamwangalia shetani.
Anyway
nadhani nimepona rohoni kwa kuwaambia habari hii , sihitaji ushauri,
nina maamuzi tayari. Huenda victim mwenyewe akipata mme mwingine
atabadilika.
By Nevile pablo-JF
No comments:
Post a Comment