Baada ya kufungashiwa virago
katika michuano ya Copa America, mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani
jana amemtembelea baba yake mzazi aliyefungwa gerezani.
Baba wa straika huyo wa PSG
alitiwa mbaroni Jumatano ya wiki hii na kuswekwa gerezani kwa kosa la
kumgonga muendesha pikipiki na alikuwa anaendesha gari akiwa amelewa
pombe kinyume na sheria.
Mtu aliyegongwa alifariki
baadaye na hii inamaanisha baba yake Cavani anakabiliwa na kosa la
mauaji na kwasasa amefungwa katika gereza la mji wa Cañitas.
Cavani alienda kumtembele baba yake jana na aliweka wazi kwamba amefanya hivyo kwa lengo la kukagua hali ya Gereza kimazingira.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizotolewa ni kwamba Cavani anafikiria kununua nyumba karibu na gereza
hilo ili awe anamtembelea baba yake kila wiki.
No comments:
Post a Comment