Akistorisha na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule
ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti
maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.
“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni
mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka
anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu barabarani
tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza kugombea,” alisema
Nape.
Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama
hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki
kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka
2010.
Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha ya
Wema ni Ndumbagwe Misayo ëTheaí (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara
Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini)
No comments:
Post a Comment