Waziri
wa Nishati na Madini George Simbachawene ameliagiza Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) kuifutia kazi Kampuni ya Selcom kwa kushindwa kutoa
huduma bora ya mfumo wa Luku.
Kutokana
na mitambo yao kutokidhi vigezo na kusababisha usumbufu kwa jamii baina
ya watumiaji wa umeme wanaonunua umeme kwa njia ya kielektronikia.
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene ameliagiza Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunja mkataba kati yao na kampuni hiyo ya
Selcom, kutokana na kero kubwa inayoletwa na kampuni hiyo na watumiaji
wa umeme kushindwa kununua umeme kwa ya kielektronikia.
Kwa
muda zaidi ya siku mbili umeme umeshindikana kununulika kwa mitandao ya
simu na mashine za Selcom, ambao ndio mawakala wakubwa wa kampuni hiyo
ya Tanesco kwa kusambaza luku nchi nzima na kusababisha watu kishinda
kiza na baadhi ya biashara kutofanyika kutokana na kukosekana kwa umeme.
No comments:
Post a Comment