Mengi yamezungumzwa kwenye mitandao na kuchukua headline kuhusu Ujauzito wa Muigizaji wa filamu, Aunt Ezekiel, Feb 2 kupitia Amplifaya ya Clouds FM 'Aunt Ezekiel' amefunguka na kujibu baadhi ya maswali haya.
Kwenye mahojiano aliyo yafanya na mtangazaji wa kipindi hicho 'Millard Ayo' ambapo aliulizwa kuhusu ndoa yake aliyo olewa na Mtanzania aishiye Dubai, Aunt Ezekiel alijibu kuwa ndoa yake bado ipo na itaendela kuwepo na still bado mume wake yupo.
Alipo ulizwa juu ya taharifa za kufungwa kwa Mume wake alikuwa na majibu haya "Sipendi
sana kukiongea hicho kwasababu kama nilivyosema mwanzo kwamba maisha
yangu binafsi uwa ni maisha binafsi ambapo yakija ya usanii yanakuwa ya
usanii, kwa hiyo hayo ni maisha yangu binafsi ila kwa kifupi sijaachika
na ndoa ipo na itaendelea kuwepo…" Alisema Aunt Ezekiel.
Pale alipo ulizwa juu ya ujauzito wa 'Moza' ambaye ni dancer wa mwimbaji wa BongoFleva Nasibu Abdul aka Diamond Platnumz kuwa kuna ukweli ndani yake, Majibu yalikuwa "Mimi
mwenyewe nasoma kwenye magazeti , nasikia kwenye radio kama wewe
unavyosema hivyo yaani lakini mimi binafsi ndio najua hii mimba ni ya
nani.." Alisema Aunt Ezekiel.
Unaweza kuyasikiliza mahojiano hayo aliyofanya na Millard Ayo hapo chini:

No comments:
Post a Comment