01 February 2015

DIAMOND AMTUSI VIBAYA MPENZI WA ZAMANI WA ZARI, KING LAWRENC

ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Zari.
ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’,  juzikati aliamua kumtolea uvivu, aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King lawrenc kwa kumuita mpuuzi anayetafuta kiki kwa vile kila kukicha kazi yake ni kumfuatafuata kwa maneno ya kejeli na kumtusi.
X wa Zari, King lawrence akipozi.
Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, staa huyo alisema mara nyingi amejitahidi kumpuuza kwa kitendo chake cha kumkejeli katika mitandao ya kijamii, lakini kitu alichogundua ni kwamba mpenzi huyo wa zamani wa Zari anataka yeye amjibu ili aweze kulikuza jina lake, kitu ambacho  ni cha kijinga.
Zarinah Hassani ‘Zari’.
“Nimejitahidi sana kukaa kimya kila anaponitusi huyu jamaa, lakini kumbuka mimi ni binadamu, najaribu kuliangalia jambo hili nagundua kwamba hana chochote cha msingi anachoongea zaidi ya matusi,  anatafuta nimjibu kitu ili apate kiki aweze kutimiza ndoto zake,” alisema Diamond na kuongeza:
“Nashukuru nimegundua hana mada ya kuzungumza katika mitandao zaidi ya mimi na Zari, ningemshauri aendelee na shughuli zake za kila siku, asihangaike na kitu asichokijua, kugombana na mimi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, mimi nawaza nifanyeje ili niweze kuitangaza nchi yangu, yeye anawaza afanyeje ili aweze kupandisha jina lake, siwezi kubishana na mpuuzi.”
Mwanaume huyo Mganda, kwa muda mwingi amekuwa akiweka picha zake, Zari na Diamond akisindikiza na maneno ya kejeli na dhihaka dhidi ya mkali huyo wa Bongo Fleva, katika kile kinachoonekana kuwa ni kushikwa na wivu.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname