Beautiful
Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amecharuka na kudai anachukizwa kwa
kiasi kikubwa na wasanii ambao wanapenda kumfanyia majungu kutokana na
chuki zao binafsi.
Akipiga
stori na paparazi wetu, Madam alisema anajua wapo wengi wanaomchukia
kutokana na sababu zisizo za msingi kwa kudai kuwa anaringa na vyovyote
vile wanavyojadili lakini hajali kwa kuwa hakuna ukweli wowote.
“Watu wenye majungu hawanisumbui kichwa kabisa nabaki nawatazama tu,
sababu sina maringo wala majivuno kwa mtu yeyote, sasa cha ajabu wengine
wanasema naringa, kwa staili hiyo hatutafika mbali maana wasanii wa
nchi za wenzetu wana umoja hawana mambo ya aina hiyo,” alisema Wema
No comments:
Post a Comment