07 February 2015

AUNT EZEKIEL AVUNJA UKIMYA KUHUSU KUPEWA MIMBA NA MHESHIMIWA WAZIRI!

Mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amevunja ukimya na kupinga vikali tetesi za ujauzito wake kuhusishwa na mmoja wa mawaziri wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibainisha kuwa jambo hilo linautesa moyo wake.

Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Dar, Aunt alifunguka kwamba, mbali na kumzushia juu ya ujauzito huo, kuwa mara ya kwanza watu asiowajua walieneza uvumi kuwa alikwenda nchini Marekani na mheshimiwa huyo lakini aliwapuuza kwa kuwa alikwenda kwa kazi yake ya sanaa. 
“Kuna binadamu hawajali maumivu ya mtu mwingine, inawezekanaje mtu aanze kuropoka kitu kizito kama hicho tena mtu na familia yake, sasa mtu ambaye ndiye muhusika wa ujauzito huu anajisikiaje?“Ukweli mimba yangu siyo ya waziri, ifahamike kuwa namheshimu sana mheshimiwa, najisikia vibaya mtu anapoeneza kitu cha namna hiyo,” alisema Aunt kwa uchungu mkubwa. 
Aunt alitiririka kwamba, mbali na uvumi huo, pia alishangazwa na baadhi ya wabunge waliothubutu kuzungumza kuhusu yeye na waziri huyo tena bungeni kwenye kujadili vitu vya msingi badala yake wanazungumza mambo ambayo hayana kichwa wala miguu. 
“Hivi inawezekana kweli kabisa wabunge ambao tunawaheshimu wanakwenda kuzungumza vitu vya ajabu bungeni?
Akiwa katika pozi. “Wamenifanya nisiwe naangalia hata hilo bunge kabisa,” alisema Aunt. 
Staa huyo alimalizia kuwa mambo hayo yanampa wakati mgumu na kumuumiza kwa sababu madai yanayozungumzwa ni mazito huku yakiwa hayana chembe ya ukweli zaidi ya kuleta mfarakano kwenye familia ya waziri huyo ambaye pia ni mbunge.
Mbali na waziri huyo, pia Aunt alikanusha kuwa mimba kubwa aliyonayo si ya yule mcheza shoo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo kama wengi wanavyodai.
Kuhusu hilo, gazeti hili lilizungumza na Mose Iyobo ambaye alisema kuwa anachojua ujauzito ni wa kwake lakini akashangazwa na uzushi usiokuwa na kichwa wala miguu.
Akiwa na shoga yake Wema Sepetu. Baadhi ya mashabiki wa Aunt waliozungumza na gazeti hili walionesha kubaki na alama ya ulizo kwamba kama Aunt anamruka Mose Iyobo na amekasirishwa na tetesi za kuhusishwa na waziri huyo ambaye ni mume wa mtu huku mumewe, Sunday Demonte akidaiwa kufungwa Dubai, je, mimba hiyo ni ya nan

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname