Wakati tukisubiri tuzo za mwanasoka bora wa dunia ambaye anategemewa
kutangazwa wiki ijayo, shirikisho la historia ya soka na takwimu (IFFHS)
limetangaza listi ya magolikipa bora 10 wa mwaka uliopita.
Katika hali ya kushangaza kabisa mchezaji bora wa klabu ya Manchester
United msimu uliopita na msimu huu unaoendelea – golikipa kinda wa
kihispaniola David De Gea hayumo kwenye orodha hiyo – jambo ambalo
limeleta mjadala mkubwa miongoni mwa wadau michezo duniani.
Golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer kwa mara nyingine ametajwa kushika nafasiya kwanza kama golikipa bora duniani.
Kwa mujibu wa takwimu za IFFHS, Neuer ameshinda kwa wastani mkubwa,
akiwa na pointi 216 huku anayemfuatia golikipa wa Chelsea Thibaut
Courtois akiwa na pointi 96.
Baada ya kuwa na wakati mzuri kwenye michuano ya kombe la dunia
magolikipa kama Keylor Navas na Claudio Bravo nao wameingia kwenye
listi hiyo.
Magolikipa wengine waliopo kwenye listi hiyo ni Buffon, Sergio Romero,
Ochoa wa Mexico, Hugo Lloris na mwafrika Vincent Enyeama kutoka
Nigeria.
Kutokuwemo kwa De Gea, Iker Casillas ambaye ni mshindi wa ubingwa wa
ulaya, Copa Del Rey na klabu bingwa ya dunia kumeleta malalamiko mengi.
No comments:
Post a Comment