Aliyekuwa mpenzi wake na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, Faiza Ally amemtupia mzazi mwenzake kuwa hamjali mwanae baada ya kuachana.
Faiza alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV ambapo alikiri kuwa kuachana na Sugu kunaendelea kumuumiza.
“Imeniathiri sana hata hailezeki,” alisema. “Naona hata nikieleza siwezi kumaliza. Imeniathiri kiasi kikubwa sana, kwa sababu na mwaka mzima kama nikipumzika kulia ni siku moja.”“Yaani inauma sana mtu ambaye ulikuwa unamuona wakati wote unaomtaka, ukimpigia simu saa yoyote hata kama akiwa kazini, akiwa bungeni labda lazima akiona simu yako hata akiwa hawezi kupokea lazima aku-text kwamba nitakupigia nipo kwenye situation hii. Lakini inafika wakati nikimpigia hapokei na hata ukimtumia meseji anakujibu baada ya siku kadhaa. Kwahiyo mimi imefika wakati nimeona kwamba hajali kwa sababu haiwezekani ukae miezi miwili mitatu hujamuona mtoto na usimpigie simu hata kusikia sauti yake,” aliongeza.

No comments:
Post a Comment