Alisoma
Shule ya Msingi ya Kaigara, 1958 -1961. Alifaulu akiwa wa kwanza
kwenda Shule ya Kati (Middle School) ya Wasichana ya Kashozi –
Kamukukubwa, 1962 -1965 (sasa ni Sekondari ya Wasichana, Hekima).
Alifaulu tena akiwa wa kwanza kujiunga na shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Rugambwa, Bukoba, 1966 – 1969.
Alisonga mbele na kujiunga na kidato cha tano Shule Bingwa ya
Wasichana ya Marian College (sasa Kilakala), Morogoro. Mwaka 1972
alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, Operesheni Tumaini, Ruvu (akiwa
pamoja na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete). Akafaulu tena na kujiunga na
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Kitivo cha Kilimo, Morogoro 1972 - 1975.
Alihitimu
akiwa ameongoza darasa lake na kupewa nishani ya Mkuu wa Chuo kwa
ushindi huo. Aliajiriwa kama Mhadhiri Mzaidizi, Idara ya Uchumi. Mwaka
huohuo (1975), alichaguliwa kwenda kusoma masomo ya juu Chuo Kikuu cha
Cornell Marekani lakini Desemba 1975 akaamua kufunga ndoa na mchumba
wake aliyekuwa amemsubiri siku nyingi amalize masomo, Hayati Balozi
Wilson KamuhabwaTibaijuka, aliyekuwa kwa wakati huo Afisa katika Ubalozi
wa Tanzania, Stockholm, Swideni.
Katika ndoa yao walijaliwa watoto wanne, Muganyizi (1976), Kemilembe (1979), Kagemulo (1986) na Kankiza (1991). Waliishi vyema hadi Mungu alipowatenganisha Mei, 2000.
Hapa ndipo alipozaliwa na kukulia.
Hapa akiwa na familia yake Moscow ubalozi wa Tanzania
Uzio wa shamba lake huko Muleba,kiasili zaidi.
Geti la kuingia kwenye nyumba yake likiwa limetengenezwa kwa mbao na makuti.
Jasiri haachi asili,kwa mbali kahawa zikiwa zimeanikwa ili zikaushwe kwa jua.
Lango kuu la kuingia ndani ya nyumba
Mandhari nzuri ya nyumba ikiwa imepambwa kwa migomba yenye ukijani
No comments:
Post a Comment