31 October 2014

TID MNYAMA HII NI NOMA SANA AISEEEE

KHALEED Mohamed maarufu kama TID ni mmoja kati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao nimewahi kufanya nao kazi kwa karibu, kiasi cha kugeuka na kuwa washkaji.
Nimemfahamu kipindi kirefu kidogo, muda mchache tu tokea alipoibuka na kibao chake kilichomtambulisha, Zeze!
Sina haja ya kurudia kuelezea kuhusu ubora wa kazi zake, kwa sababu kama ni kuimba, anajua.Na najua wengi wanatambua ukali wa vibao vyake vingi ambavyo amevifanya na kumfanya kuwa mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao wameendelea kubakia katika levo za juu, katika kipindi ambacho kuna ushindani mkubwa, hasa kutoka kwa vijana wadogo wenye njaa ya mafanikio. 
TID, licha ya umaarufu wake, ameendelea kuishi maisha yake yaleyale ya uswahilini na mpaka miaka ya hivi karibuni, alikuwa bado anaishi nyumbani kwao, mitaa ya Kinondoni. Mara kibao utamkuta ametulia maskani, akiwa na washkaji wa miaka yote, tofauti kabisa na baadhi ya mastaa ninaowajua, ambao umaarufu uliwahamisha na kuwatenganisha na watu wao wa zamani. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname