Akionekana ni mwenye ngozi nyororo na umbo lenye mvuto kama
mshambuliaji wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, kijana
anaetambulika kwa jina Joe Weller, amekua akiwahadaa wasichana kwa
kujifafanisha na Cristiano Ronaldo.
Kijana huyo amekuwa akifanya matukio ya kuwahadaa watu hususana
wasichama, katika mji wa Brighton uliopo kusini mwa Uingereza ambapo
mara kadhaa wasichana wamekua wakivutiwa nae na kufikia hatua ya
kumtamani kutokana na mvuto wake.
Hata hivyo wasichama wengi wamekuwa wakiamini kijana huyo ndio Ronaldo
wa ukweli, kutoka kwenye klabu ya Real Madrid kwa namna anavyovaa na
muonekano wake na pia hutumia matamshi ya maneno ya lugha ya kireno.
Mbali na hivyo wasichama wengine hufika mbali zaidi kwa kutaka kumbusu
na kumkumbatia ikiwa ni sehemu ya kutaka kuonyesha hisia zao kimapenzi
kwa Cristoano Ronaldo ambaye inasemakana hupata wakati mgumu
anapokutana na wakinadada mitaani.
No comments:
Post a Comment