02 October 2014

100.5 Times Fm kumleta Davido Tanzania, November 1

Msanii wa Nigeria anaetamba na hits kibao, Davido ataingia Tanzania mwishoni mwa mwezi huu na kufanya show kubwa November 1.
Msanii  huyo analetwa na kituo cha radio cha 100.5 Times Fm kupitia tamasha lake jipya lililopewa jina la ‘The Climax’.
Tayari vidokezo vya show hiyo vimeanza kurushwa kwenye kituo  cha radio huku orodha ya mengi yatakayofanyika ikitarajiwa kuwekwa wazi muda wowote kuanzia leo.

Davido ambaye ni mshindi wa tuzo kadhaa kubwa ikiwemo tuzo ya BET na MTV (MAMA) anatamba na hits kadhaa ikiwemo Skelewu, Aye, tchelete na nyingine nyingi.

 
Kaa mkao wa kushangweka na kilele cha burudani cha mwaka ‘The Climax’ ya 100.5 Times FM.Muziki Wetu Afrika Yetu.
“Paris was Great next stop!! LONDON –LAGOS-WARRI-SOUTH AFRICA-NAMIBIA-TANZANIA lego.” Ameandika Davido kwenye Instagram.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname