23 October 2014

AJALI NYINGINE IRINGA.



Muonekano wa basi la Florida baada ya ajali hiyo kutokea.

Basi la Kimotco likiwa pembezoni mwa barabara baada ya ajali hiyo.

Polisi na mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
Abiria waliokuwa wakisafiri katika mabasi ya Kimotco na Florida leo asubuhi walinusurika baada mabasi hayo kugongana uso kwa uso katika barabara ya Iringa-Dodoma leo saa moja na nusu asubuhi. Basi la Kimotco husafiri kati ya Iringa na Arusha na lina namba za usajili T449 CAL wakati Florida  husafiri  kati ya Migoli  na Iringa na lina namba za usajili T571 BDX.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo  ilisababishwa na kona katika eneo husika na mwedo kasi wa mabasi yote mawili.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname