Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari.
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekana shutuma zilizoelekezewa kwao
kuwa wanahusika na kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel
Ten, Daudi Mwangosi.Baadhi
ya viongozi wa Chadema kutoka kushoto ni Ofisa Habari, Tumaini Makene,
Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika, Ofisa Mwandamizi Mafunzo na
Uendeshaji, Mohamed Mtoi, na mwenye gwanda ni Katibu Mtendaji, Ofisi ya
Katibu Mkuu, Victor Kimesera.
Mkurugenzi
wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Mhe. John Mnyika, ameeleza kuwa
hawahusiki na mauaji hayo bali ni propaganda zinazoenezwa ili
kuwasahaulisha wananchi juu ya suala la katiba linaloendelea.
Mnyika
alieleza kuwa wanaoeneza habari hizo ni wale ambao wanataka kuizuia
Chadema na Ukawa kwa ujumla kuendelea na harakati za kupigania katiba ya
wananchi ikiwemo kufanyika maandamano ya kitaifa iwapo Rais Kikwete
hataingilia kati kulisimamisha zoezi la katiba mpya.
No comments:
Post a Comment