26 June 2014

JE, WEWE NI MMOJA WA VIJANA WENYE TATIZO LA KUJICHUA AU UNAMFAHAMU MWENZAKO MWENYE TABIA HIYO? SOMA HAPA UJIELIMSHE



Leo naomba nizungumzie tatizo ambalo nahisi vijana wengi tumekuwa watuhumiwa katika kitendo hiki.
Kujichua ni tabia ya kingono ambayo inapofanywa kwa kiwango kikubwa inaleta matatizo ya kiumbo na kisaikolojia kwa anayefanya tendo hilo.
Na katika kipindi cha zama hizi ambazo majarida, vipindi na hata mitandao mingi inaonyesha picha za ngono ndio kunaifanya tabia hii kushamiri kwa kiwango kikubwa.
Kwani vijana wengi wanaingia katika mchezo huu wa kujiridhisha wenyewe bila kujua madhara yatakayokuja baadaye.

Waelimisha rika wengi wamekuwa wakiwaambia vijana kwamba kujichua ndio njia salama ya ngono kwani hatari ya kupata magonjwa kwako haipo na wanaongezea kuwa wafanye kwa kiwango kidogo pale wanapojisikia hamu ya tendo.
Lakini wanasahau kuwaeleza madhara yake pindi inapofanywa kwa kiwango kikubwa na pia wanajua wazi kuwa mara mtu anapoanza tabia hii kuitawala kwa kiwango inakuwa ngumu.

Baadhi ya madhara ambayo unaweza ukayapata ukifanya kwa muda mrefu:
1.Maumivu ya mgongo kwa chini;
2.Kupoteza nywele;
3.Kupungua nguvu za kiume;
4.Kuwahi kumaliza wakati wa tendo; 
5.Kupoteza uwezo wa kuona vizuri;
6.Maumivu ya kende;
7.Maumivu ya nyonga;
8.Kuchoka sana;
9.Msongo wa mawazo;
10.Kupoteza kumbukumbu kwa haraka

Dhumuni la makala hii ni kumsaidia yule mtu ambaye tayari anafanya mchezo huu atambue madhara yake na pia afahamu namna ya kujinasua kabla mambo hayajawa mabaya.
Kwa wewe muhusika unatakiwa kuwa na hakika kuwa unaweza ukajinasua katika tatizo lako hili. 
Wengi wanaume kwa wanawake waliojaribu kujisaidia kuondokana na hili tatizo wameweza,  hata wewe kwako ni hivyo hivyo ikiwa utajitambua tu.
Kujitambua ni hatua ya kwanza katika safari yako ya kuacha.
Unatakiwa uamue kuwa sasa unaacha na pindi unapoweka uamuzi huo utakuwa unasaidia kujipunguzia ukubwa wa tatizo.
Lakini inatakiwa uwe na zaidi ya tumaini au tamanio la kutambua kuwa uamuzi wa kuacha ni muhimu kwako.
Ni uamuzi tu.
Ukiweka kweli kabisa mawazo yako katika kuliondoa hili tatizo utakuwa na nguvu ya kuweza kuliondoa kabisa na kujiweka pembeni na vishawishi vya kukurudisha katika hiyo tabia.

Utakapo kuwa ushafanya uamuzi wa kuacha anza kufanya yafuatayo:
1.Usiguse wala kuchezea maeneo yako ya siri kwa muda mrefu labda uwe unajisafisha wakati wa kuoga.

2.Tengana na rafiki au marafiki zako ambao unajua wazi kabisa kuwa nao wana tabia hizo kwani usijidanganye kuwa mtaacha wote kwa pamoja kwani mara nyingi kuacha ni juhudi na maamuzi binafsi.

3.Unapokuwa unaoga usikae muda mrefu maeneo hayo jifute na utoke haraka.

4.Lala na nguo inayozifunika sehemu za siri kiasi kwamba sio rahisi kwa wewe kuzigusa mpaka uivue hiyo nguo, hapa itakusaidia kupata muda wa kutafakari kabla hujafanya tendo lolote.

5.Endapo upo kitandani na mawazo ya tendo hilo yakakujia ,nyanyuka na ujaribu kutembea tembea ili kuyapoteza hayo mawazo kichwani mwako.

6.Usisome majarida ya ngono, na kuangalia picha za ngono kwani vitakuchochea urudi katika tatizo.

7.Anza kusoma majarida na makala za mambo mazuri na yenye kuelimisha na itakusaidia kuulisha ubongo taarifa nzuri. 
Mathalani unaweza ukaanza tabia ya kusoma vitabu vya dini itakuasidia sana.

8.Sali, lakini wakati wa kusali usiwe mara kwa mara unalifikiria hili tatizo kwani utaendelea kuliweka mawazoni mwako.

Mtazamo wa mtu mwenyewe ndio unaosaidia kuliondoa hili tatizo kwa haraka.
Ukiweza kutambua kwanini umeingia katika hii tabia, 
na kuyafahamu mazingira yanayokuchochea wewe kuingia huko unatengeneza uwezo wa kuishinda kwa haraka.

 Tabia hii ya kujiridhisha mwenyewe itakufanya uwe mtu kwa kujisikia na hatia kila mara, kutojiheshimu mwenyewe na kukufanya uendelee pindi unapopatwa na msongo wa mawazo.
Na inapelekea unaanza kujiona mdhambi hata kuhudhuria nyumba za ibada kwako inakuwa ngumu.

UAMUZI WA KUACHA UNAWEZA KUUFANYA SASA
KWAAJILI YA AFYA YAKO YA UZAZI NA AKILI.

ANZA JUHUDI NA UTAONA JINSI UNAVYOWEZA KUISHI BILA TABIA HIYO AMBAYO HAINA FAIDA YOYOTE SIKU ZA BAADAYE

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname