NBA
imesema kutokana na uchunguzi kukamilika kuhusu mmiliki wa timu ya Las
Angeles Clippers Donald Sterling dhidi ya maneno ya kibaguzi kwa watu
weusi, imempa kifungo cha maisha mmiliki huyo mwenye umri wa miaka
80.Wanasema baada ya kufanya uchunguzi Donald amekubali kwamba sauti
iliyosikika ikitoa maneno mazito ya kibaguzi dhidi ya watu weusi ni ya
kwake ambapo alikua akiongea na Mwanamke anaedaiwa kuwa mpenzi wake.
Donald
ambae aliwahi kukiri siku kadhaa zilizopita kwamba hatoiuza hii timu,
kwenye adhabu ya maisha aliyopewa ni kwamba hatoruhusiwa kuhudhuria
mazoezi ya timu yake wala kwenda kwenye game zote maishani mwake na
vilevile hatoruhusiwa kufanya maamuzi yoyote kwenye timu.
Kingine kilichoongezeka ni faini ya dola za Kimarekani milioni 2.5 ambazo kibongobongo inagonga kwenye 4107500000 ambapo
inasemekama hii sauti ya Sterling akitoa maneno ya kibaguzi ilirekodiwa
September 2013 na kwamba alishtukia kwamba karekodiwa.
No comments:
Post a Comment