Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja
iwapo trafiki huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo
kituo cha polisi, alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati
anapelekwa hospitali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi huyo alikufa ghafla akiwa kazini
lakini alikataa kuingia kwa undani wa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati
ya saa 5:00 asubuhi na saa 6:00 mchana, baada ya trafiki huyo kukamata
daladala linalofanya kazi zake kati ya Kiborloni na katikati ya mji.
Mmoja wa mashuhuda alisema :“Baada
ya kuikamata hiyo Hiace (Toyota) pale Kiborloni aliingia kwenye hiyo
gari na kukaa kiti cha mbele pembeni ya dereva na kumwamuru kulipeleka
kituoni.
“Wakati wakiwa njiani kuelekea
kituoni ghafla yule trafiki akawa haongei na akawa anamwegemea dereva…
hiyo hali iliendelea hadi walipofika kituoni ndipo dereva akawaeleza
trafiki wenzake.”
Mwili wa polisi huyo ulisafirishwa juzi kwenda Mbeya kwa mazishi
Mwili wa polisi huyo ulisafirishwa juzi kwenda Mbeya kwa mazishi
No comments:
Post a Comment