21 April 2014

MBEYA CITY YAAGIZA NDEGE YA CHINI...


MBEYA City imemaliza Ligi Kuu Bara kwa kushika nafasi ya tatu na sasa imeanza kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao kwa maana na usajili pamoja na kutengeneza miundombinu yake, likiwamo suala la usafiri kwa kununu basi la kisasa litakalokuwa ‘ndege ya chini’.
Mikakati mingine ya miundombinu hiyo ni kujenga uwanja wao. Kwa suala la uwanja, inatarajia kuanzisha kazi ya kuujenga katika eneo la Iwambi mjini Mbeya. Eneo lao limeelezewa kuwa na ukubwa ekari 15.
Ukija kwenye suala la usafiri ambalo linatarajia kukamilika muda si mrefu kutoka sasa, klabu hiyo inatarajia kununua basi jipya la kisasa lenye huduma zote ndani. Basi hilo litakuwa ama Yutong au Higer.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, ameliambia Mwanaspoti kuwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambayo ndiyo mmiliki wa timu hiyo, imeshatangaza tenda kwa kampuni mbalimbali zinazouza magari baada ya kuweka wazi sifa za basi wanalolihitaji.
“Tulitangaza mara ya kwanza, hakukuwa na kampuni iliyojitokeza, tukarudia ndipo kampuni tatu zimejitokeza na hivyo itapendekezwa kampuni moja kulingana na makubaliano yatakayofanyika,” alisema Kimbe.

“Tupo katika hatua za mwisho za ununuzi wa basi la timu, tutahitaji moja lenye hadhi tunayoitaka, fedha zipo.”
Source.. Mwanaspoti

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname