Miezi ikapita, mawiki yakasonga hatimae
siku, masaa na dakika zake zikapotea na sasa EFM inayopatikana katika
masafa ya 93.7 imesikika hewani kwa majaribio kwa mara ya kwanza.
Redio hii iliobeba watangazaji mahiri,
waandaaji wa vipindi wenye umakini, ma DJ wanao sadikiwa kuwa
walishushwa kwa ajili ya kazi hii, uongozi thabiti na yenye usikivu
mujarab, habari zake zilianza kupenya kwenye masikio ya washashi
mwishoni mwa mwaka jana na kupelekea wamiliki na wadau wa redio nyengine
kukosa usingizi na hata siku wakiupata basi huweweseka usiku na kupiga
mayowe ama kujikuta wakikosa hata nguvu ya kuzuia haja ndogo kutoka.
Redio hii itadili kwa asilimia 85 na
burudani...na watakaoongoza balaa hilo ni watu wenye kulijuwa game kwa
kipindi kirefu saana na burudani iliolengwa hapa hakika ndio mwiba
mchungu utaowatesa weengi waliowanyonya na kuwanyanyasa wasanii kwa
miongo kadhaa sasa.
Kuna Minong'ono kuwa inamilikiwa na Lady Jay Dee....Kwa mwenye Ukweli Funguka Hapa basiiiii....
No comments:
Post a Comment