30 April 2014

MATESO YA DUNIA!! ANA MIAKA 31, HAJAWAHI KUTEMBEA HATA SIKU MOJA



Mateso juu ya mateso! Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Grace Mkondora mkazi wa Mabibo Farasi, Dar anateseka na uti wa mgongo tangu alipozaliwa.Grace (31) anayeishi na mama yake, Mary Liyoya alizaliwa kabla ya muda wake (Miezi 8) na alipozaliwa alikuwa na uzito wa kilo moja tu.Hali yake ilianza kuwa tofauti tangu akiwa mdogo ambapo alikuwa hawezi hata kucheza wala kuongea chochote.Mama Grace akisaidiana na mumewe, Flumance Mkondora waliweza kumpeleka Grace katika hospitali mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa, Muhimbili pasipo kufanikiwa kupata tiba yoyote.

kati ya hospitali nyingi walizompeleka walikuwa wakikatishwa tamaa na kuambiwa mara hawezi kupona tena, wengine wakisema kuwa ameshakuwa tahaira hawezi kupona milele, lakini kwa hilo mama Grace alipingana nalo na wala hakukata tamaa na maisha.
Kuna kipindi walishampeleka katika maombi kwenye makanisa mbalimbali lakini hakukuwa na matarajio yoyote.
Alipofikisha umri wa miaka 20, hali ya Grace ilizidi kuwa mbaya zaidi kwani kwa kipindi hicho alikuwa akitokwa sana na mapovu mdomoni na kujikunja mara kwa mara na hata kuongea kwake kulikuwa ni kwa shida zaidi kutokana na ulimi wake kuwa mzito.
Waliamua kumpeleka tena katika Hospitali ya CCBRT na alipofikishwa kwa ajili ya vipimo madaktari walimwambia kuwa umri umeshakwenda hivyo viungo vimekomaa na hawezi kupata matibabu ya kurekebishwa mgongo.
Baada ya majibu hayo walimpeleka moja kwa moja katika Kituo cha Masista ambapo hulelewa watu wenye ulemavu nakumuweka kwa miezi mitatu chini ya uangalizi wa masista.Mama Grace anasimulia zaidi kuwa baada ya kupita miezi hiyo waliamua kumchukua mtoto wao na kurudi naye nyumbani mpaka sasa.

Mpaka sasa Grace anaishi na wazazi wake akiwa katika wakati mgumu, muda wote kitandani hajielewi, analishwa chakula, huduma zote za kujisaidia zinafanywa na mama yake.
Kama umeguswa na unahitaji kumsaidia Grace kwa namna yeyote ile usisite.

Mtumie chochote kupitia namba hizi:

Mama yake, 0765 150 423 Mary Liyoya
Baba yake, 0754 311 940 Flumance Mkondora

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname