NBA
imesema kutokana na uchunguzi kukamilika kuhusu mmiliki wa timu ya Las
Angeles Clippers Donald Sterling dhidi ya maneno ya kibaguzi kwa watu
weusi, imempa kifungo cha maisha mmiliki huyo mwenye umri wa miaka
80.Wanasema baada ya kufanya uchunguzi Donald amekubali kwamba sauti iliyosikika ikitoa maneno mazito ya kibaguzi dhidi ya watu weusi ni ya kwake ambapo alikua akiongea na Mwanamke anaedaiwa kuwa mpenzi wake.
80.Wanasema baada ya kufanya uchunguzi Donald amekubali kwamba sauti iliyosikika ikitoa maneno mazito ya kibaguzi dhidi ya watu weusi ni ya kwake ambapo alikua akiongea na Mwanamke anaedaiwa kuwa mpenzi wake.
Donald ambae
aliwahi kukiri siku kadhaa zilizopita kwamba hatoiuza hii timu, kwenye
adhabu ya maisha aliyopewa ni kwamba hatoruhusiwa kuhudhuria mazoezi ya
timu yake wala kwenda kwenye game zote maishani mwake na vilevile
hatoruhusiwa kufanya maamuzi yoyote kwenye timu.
Kingine kilichoongezeka ni faini ya dola za Kimarekani milioni 2.5 ambazo kibongobongo inagonga kwenye 4107500000 ambapo
inasemekama hii sauti ya Sterling akitoa maneno ya kibaguzi ilirekodiwa
September 2013 na kwamba alishtukia kwamba karekodiwa.
Yote haya
yametokana na kuvuja kwa sauti ya mazungumzo kati yake na girlfriend
ambapo Donald Sterling aliongea maneno makali ya kibaguzi kwa kusema
kwamba hataki girlfriend wake ajihusishe na watu weusi kwa kupiga picha
au kwenda nao kwenye mechi.
Imeshangaza
zaidi kwa sababu timu yake ina wachezaji mashuhuri weusi kama Chris
Paul na Blake Griffin aliyewahi kucheza ligi ya chuo pamoja na Mtanzania
Hasheem Thabeet lakini wakiwa wanatoka kwenye vyuo tofauti.
Kamishna wa NBA amesema atatumia nguvu ya uongozi wake kuhakikisha L.A Clippers haimilikiwi tena na Donald Sterling.
Video ya mazungumzo yote iko hapa chini kama ulimis
No comments:
Post a Comment