17 April 2014

KAULI YA KWANZA YA MBOWE AFAFANUA UKAWA KUONDOKA BUNGENI

 Mh Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya bunge maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa wananchi.
Mheshimiwa Mbowe ameeleza jinsi ambavyo bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa sana,Matusi makubwa ya nguoni kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya serikali ya ccm,kutumia vitisho vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .

Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano kwamba Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba kama serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo kwanza vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.BOFYA KUSOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname