16 February 2014

HAYA NDO MAPOZI 11 ya kwenye simu yanayotumiwa na wanawake kuwanasa wanaume...!


Hili ni pozi la mwanamke akisubiri simu ipokelewe, kuna kitu anata kumweleza mpenzi wake na anasubiri apokee simu kwa shauku kubwa..........


Ukiona mwanamke anaongea na simu kwa pozi hili jua hapo mwanaume anataka kuingizwa Kingi na hatochomoa...
Hili ni pozi ambalo huendana na mirindimo ya sauti ya kubembeleza kwa maneno matamu na yenye kuleta ashki kwa mwanaume....



Hili ni pozi la kumnasa mume wa mtu, hapo unaweza kukuta anahimizwa apitie nyumba ndogo kabla ya kwenda kwa mkewe na akithubutu huenda siku hiyo mwanaume akauza mechi na nyumbani asirudi. Maana atakutana na maandalizi ambayo yatamfanya apoteze network kwa muda na akishtuka kumekucha .......


Hili ni pozi la kukumbushia mechi ya jana jinsi ilivyonoga. Hili pozi likinogeshwa na sauti ya mahaba yenye lafudhi ya pwani, lazima mwaume aingie kingi.


Hili pozi la kuomba hela ya shopping, mwanaume lazima atoe hela atake asitake.......................


Hili ni pozi la kukumbushia mtoko (dates)..............


Hili pozi hutumiwa na wanawake kuwashawishi wapenzi wao wawahi kurudi nyumbani mapema maana wana hamu nao......


Hili pozi hutumiwa na wanawake kuwaaandaa wenzi wao kimapenzi kabla ya mechi, hapo mwanaume lazima ajue akirudi nyumbani ligwaride linamsubiri.........


Hili pozi feki la kukataa mtoko wa mwanaume wakati anataka, hapo mwanamke anajifaragua kujifanya ana ratiba nyingine na hawezi kubadilisha, lakini hapo anaomba Mungu jamaa akaze uzi kusisitiza ili ajifanye anakubali kwa shingo upande kumbe moyoni ana lake jambo. Kama mwanaume akikubali kwamba watapanga siku nyingine itamuumaje, maana halikuwa lengo lake kukataa bali alikuwa anataka kutingisha kibiriti tu, ili kujua kwamba mwanaume anampnda kiasi gani... Wanaume tuna kazi.....!!!


Hili ni pozi la kusubiri simu ya mwanaume aliyekuwa na mtoko naye. Kwa kawaida baada ya mwanamke kuwa na mtoko na mwanaume hutarajia kupigiwa simu baada ya kila mtu kurudi kwake, lakini akiona kimya hapigiwi simu maswali mengi huenda kichwani kwa mwanamke. Je hajavutiwa na mimi? Je kuna kitu nimemuudhi? Je mimi sio kiwango chake? ilimradi atajiuliza maswali lukuki. Ikitokea hajapigiwa simu kabisa hatolala usiku kucha akijiuliza maswali yasiyo na majibu. Nawasihi wanaume wakiwa na mtoko na mwanamke hata kama hajampenda apige tu simu kumtakia usiku mwema kwani kumchunia baada ya mtoko ni kumuumiza mwenzake kihisia na kumpa jakamoyo....


Hili ni pozi linalotumiwa na wanawake kutunga uongo. Hapo labda mwanaume anapiga simu na anajua anataka nini, kwa sababu hana uhakika ajibu kitu gani anajaribu kutafuta jibu la uongo ili kuepusha shari.......

 
watu8 ukiona mwanamke ameweka pozi kama hili wakti anaongea na simu jua kwamba anatongozwa na hapo mwanume anashusha mashairi, lakini mwanamke anakuwa hana uhakika kama mwanaume huyo ni mkweli aua anadanganywa. Hilo pozi limekaa ki fifty fifty yaani akubaliau akatae, inawezekana ni kuombwa mtoko lakini nia imeshajulikana na mwanamke anashindwa kujua akubali au asikubali.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname