Baada ya kukubali dili la kumuuza kiungo kutoka nchini Hispania Juan Manuel Mata García kwenye
klabu ya Man Utd, uongozi wa klabu ya Chelsea unajipanga kuwapiga kumbo
majogoo wa jiji Liverpool katika harakati za kumuwani mshambuliaji wa
pembeni kutoka nyumbani Afrika katika nchini ya Misri Mohamed Salah.
Chelsea wamejipanga kufanya hivyo huku wakiamini fedha watakazozipata katika mauzo ya Juan Mata zitakuwa kivutio kizuri kwa uongozi wa Fc Basel, kwa kumpata Mohamed Salah ambae tathmini yake haizidi Euro million 20.
Liverpool ndio walikuwa wa kwanza kuonyesha nia ya kutaka kumsajili winga huyo kutoka nchini Misri, lakini ofa yao iliyowasilishwa huko Nchini Uswiz mwanzoni mwa mwaka huu ilikataliwa na viongozi wa Fc basel kwa madai ilikua haikidhi thamani ya Mohamed Salah.
Chelsea wamevutiwa na Mohamed Salah, baada ya kumuona akicheza vyema wakati wa michezo ya hatua ya makundi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo Fc Basel waliifunga mara mbili The Blues katika hatua hiyo huku katika mchezo wa pili uliochezwa mjini Basel mshambuliaji huyo ndie aliifungia klabu yake bao la ushindi.
Wakati huo huo kiungo kutoka nchini Hispania Juan Mata hii leo alitarajia kupimwa afya yake huko Old Trafford kabla ya kukamilisha taratibu nyingine za kujiunga na klabu ya Man Utd.
Chelsea wamekubali kumuuza Juan Mata kwenye klabu ya Man Utd kwa ada ya uhamisho wa paund million 37,ikiwa ni faida ya paund million 11 kufutia kiasi cha pesa walichokitumia wakati wakimsajili akitokea Valencia mwaka 2011 ambapo The blues iliwatoa paund million 28.7.

No comments:
Post a Comment