Meneja mpya wa Manchester United, David
Moyes anaendelea kukabiliwa na kibarua kizito kutokana na kikosi chake
kuendelea kufanya vibaya tangu akabidhiwe mikoba na meneja wa zamani,
Alex Ferguson. Hii ni baada ya kijana mmoja anayeaminika kuwa shabiki wa timu hiyo kujiua juzi. Dec 7 jijini Nairobi, Kenya baada ya timu yake kufungwa 1-0 na Newcastle.Polisi wamesema kijana huyo aitwaye, John Jimmy Macharia, 23, alijirusha kutoka ghorofa ya 7 baada ya kujua timu yake imepoteza mchezo huo. “Mashahidi wote waliokuwepo wakati wa tukio bado wapo mikononi mwa polisi wanahojiwa,” alisema. Naye rafiki wa karibu wa marehemu alisema kabla ya kuanza kwa mpira marehemu John ,aliwaambia rafiki zake yeye hawezi kuangalia game kwenye banda la video anaenda kuangalia nyumbani kwake. Source:KTN
No comments:
Post a Comment