29 December 2013

HUU NDIO UKWELI KUHUSU DIAMOND....HAMNA WA KUCHEZA LIGI MOJA NAE SASA HIVI...!SOMA ZAIDI HAPA...

Ni msanii gani anayecheza ligi moja na Diamond Platnumz sasa hivi? Naamini yupo kwenye ligi yake mwenyewe na hadi sasa hana mpinzani. Japokuwa kama ni mpira wa miguu, Diamond anaweza kuwa kwenye ligi kuu pamoja na timu zingine (wasanii wenzie) kwa anachokifanya, anaweza kuwa kwenye ligi kuu plus ambayo hakuna msanii mwingine anayefikia matawi yake.

Kutoka kwenye historia ndefu iliyokumbwa na umaskini wa kutupa enzi za utoto na ujana wake kabla hajatusua, hadi kufikia kuwa msanii tajiri, anayetafutwa kuliko wote kwaajili ya show na anayelipwa fedha nyingi zaidi kuliko wote. Kutoka kwenye maisha ya kudhauliwa, kufanya kazi kwenye viwanda na ujira wa shilingi 3,000 kwa siku, hadi kuwa msanii anayeingiza si chini ya shilingi milioni 40 kila wiki. Hakuna msanii anayependwa zaidi nchini kwa sasa kumzidi. 

Pamoja na sifa nzuri za kuwa hitmaker maisha yake upande wa pili yamekuwa yakiandamwa na scandal nyingi. Amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengi warembo na wenye majina ambao wengi wao ameishia kuwavunja roho kutokana na kutokuwa mwaminifu kwenye uhusiano wake. 

Japo anasema amewahi kuumizwa sana na Wema Sepetu aliyemtuhumu kwa kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao, Wema pia anasema amewahi kuumizwa mara nyingi na Diamond. Kwa maana nyingine ni kuwa, Diamond na Wema wana mambo mengi wanayofanana; wote ni heartbreakers. 

Wema na Diamond wamekuwa na uhusiano wa on and off kwa kipindi kirefu. Pamoja na wakati mwingine kila mmoja kuamua kuendelea na maisha yake, wapenzi hawa wameendelea kuhook up kisirisiri na kuendelea kulila tunda lao. Mara ya kwanza wameachana, Wema ndiye aliyemshutumu mwenzi kwa kumsaliti.
clip_image001[8]
“Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate,” Wema aliliambia gazeti la Mzuka katikati ya mwaka huu. “Nilikuwa sijui and maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye.

Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha akaendelea na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu.” Kipindi Diamond anakutana na Jokate, mrembo huyo alikuwa tayari yupo kwenye uhusiano na mchezaji wa ligi ya NBA, Hasheem Thabeet. Uhusiano wao ulikuwa umedumu kwa miaka miwili na Jokate alikiri kuwa alikuwa akimpenda sana mchezaji huyo. Hata hivyo muda huo umbali wao na matatizo ya hapa na pale ukamfanya Jokate awe kwenye hali ya upweke na hivyo kumpa nafasi Diamond.
clip_image001[6]“Kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi. Ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali,” Jokate aliliambia gazeti la Ijumaa Wikienda October mwaka huu.

Hata hivyo, Jokate alijikuta miongoni mwa wasichana wengi waliyoumizwa na Diamond baada ya kuwa naye kwa kipindi cha miezi miwili tu.

Kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, cha katikati ya mwaka huu, Diamond alikiri kumuuliza Jokate.

“Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea,” alisema Diamond.

Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”

Bongo5 iliwasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond na kusema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli. “Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” alisema Jokate.

Pamoja na kuachana huko kulikoonesha ishara ya kutorudiana tena, Diamond na Wema waliendelea kuwa na ukaribu ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa ukiwaumiza wengi. Msichana aliyekuja kuumizwa zaidi ni Penny ambaye kwake Diamond alikuwa mwanaume wa kipekee.
clip_image001“Lakini I will tell you one thing, Diamond is an amazing person, whatever you see anachofanya, whether he is kissing, he is talking to me, whether ananichekesha, yaani he is a five star. So you can imagine ilikuaje. It was weird but very good; everything about him is just amazing,” Jokate aliliambia jarida la Mzuka.

 Aliliambia jinsi ambavyo Diamond alikuwa akimfanyia surprise nyingi na mapenzi tele.

“The first one I think is buying me a car coz sikuexpect, I didn’t see it coming, ilikuwa out of the blue. Unajua tumeshazoea kwamba watu wanaofanya vitu hivi ni wanaume wakubwa, wababa mpaka uhongwe umehongwa na mtu mzima lakini for Diamond amesema hivyo tu ghafla…. nilikuwa sijui natoka naenda wapi akaniambia hebu njoo nikuambie he said, ‘I got you a car, he gave me money akasema go and buy that car,” alisema na kuongeza kuwa Diamond alimkabidhi shilingi milioni 15 kununua gari hilo.

“He said go buy this car. Ananiulizaga, he is very funny’ unapenda gari fulani mi’ mimi najibu yeah I like it’. I was so shocked, ghafla so I think that’s the first surprise. He is too sweet; kwanza he will come take you out for a dinner out of the blue. Yaani anafanya vitu ambavyo kwa age yake na persona yake vilivyo alivyo an artist unategemea awe ghetto, ‘ebwana uko wapi twenzetu pale tukapige kiepe’ unajua vile. But he is very sweet that surprises me, he surprises me I think every day. Na anachonisurprise kingine kikubwa I will tell you guys, ni uwezo wake wa kufikiri, he is very smart.”  

Bahati mbaya kuamini huko kumekuja kugeuka baada ya hivi karibuni Diamond kurudiana na Wema Sepetu na ukweli huo ulibainika baada ya kuvuja picha zao wakiwa Hong Kong hivi karibuni. Tukio hilo liliuvunja vibaya moyo wa Penny ambaye tayari alikuwa akiishi na Diamond na nyumbani kwao alikuwa akijulikana na mchumba aliyepitishwa na familia nzima akiwemo mama yake Diamond na dada zake.

Usaliti huo ulipelekea mgogoro mkubwa kati ya Diamond na Penny ambaye kuna tayari kuna tetesi kuwa wameshaachana rasmi. Tangu hapo Wema amekuwa haoni aibu kuonesha mapenzi yake kwa Diamond ikiwa ni pamoja na kupromote show ya Diamond ya Christmas.

Kwenye show hiyo ya Jumatano hii ndipo mambo yalipowekwa wazi zaidi ambapo Wema alikuwa mmoja wa watu waliopanda kwenye stage na kuongea na watoto waliokuwa wakishuhudia show. Kwenye show hiyo Diamond alisikika akiuliza: Mnataka kumjua mchumba wangu”? Baadaye wakati akitaka kuimba wimbo wake ‘Ukimwona’, hitmaker huyo aliuliza tena: Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani,” na ndipo Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.

Baada ya Penny, hatujui ni msichana gani atakayevunjwa tena moyo na Diamond kutokana na kuendelea kwa uhusiano usiokatika na Wema kama vile wamekula yamini.
 SOURCE: BONGO 5

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname