20 November 2013

MAINDA ATISHIWA KUUAWA..BAADA YA KUONGEA UKWELI JUU YA MAHUSIANO YAKE NA RAY NA KUWAVUA NGUA JOHARI NA CHUCHU HANSI KWA KUVAMIA MAHUSIANO YAKE

 
 Baada ya staa wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kufunguka  kuhusu mambo mazito yaliyomo ndani ya tasnia ya filamu, staa huyo ameanza kupokea vitisho vya kukatishwa uhai wake.



Kwa mujibu wa watu walio karibu na Mainda, staa huyo amekuwa akiandamwa na simu za vitisho zinazomtaka kuacha kuongelea habari zao la sivyo watamteka na kumfanyia kitu mbaya.
 
Baadhi ya wasanii wamekuwa wakimuoneshea vidole staa huyo kwa mambo mawili, wengine wakimuona kama ni jasiri na wengine wakiwa na chuki naye.
 
“Kuna baadhi ya watu wanamsifu Mainda na wengine wanamsema vibaya kiasi cha kumwambia kwamba siku zake za kuishi zinahesabika,” alisema mmoja wa watu hao.
Mbali na Mainda kutoboa uhusiano wake wa kimapenzi na Ray, pia aliweka wazi jinsi wasanii wenzake, Blandina Chagula ‘Johari na Chuchu Hans, walivyomuingilia kwenye penzi lake hilo.
 
Aidha, msanii huyo ambaye pia hupenda kujiita Small Baby aliliponda kundi la Bongo Movie Unit kwa kusema kuwa limejaa uchafu.
 
Kupitia gazeti la Risasi Mchanganyiko lililowasaka Ray, Johari na Chuhu ili kuweza kupata mzani wa habari kuhusiana na kile alichokiongea Mainda lakini wasanii hao wamekuwa wakiogopa kusema chochote.
 
Katika hali ya kuonesha kumhofia Mainda, Ray amekacha miadi na mwandishi wetu mara kadhaa.
 
Naye Johari amekuwa akisema kwamba Mainda amewavua nguo huku akikataa kufunguka zaidi.
 
Kwa upande wake, Chuchu amekuwa akigoma hata kupokea simu za waandishi wetu.
Tulipomtafuta Mainda alisema hakuna kitu anachokiogopa chini ya jua.
“Kwanza sioni kibaya nilichokiongea, bado nina mambo mengi zaidi ya hayo,” alisema staa huyo na kuongeza kwamba hakuna mtu wa kumziba mdomo.
 “Ninachoweza kuwaambia ni kwamba niko tayari kufia kwenye mapambano, sitaogopa chochote,” alisema Mainda

GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname