20 November 2013

50 wafukiwa baada ya jengo kuporomoka Afrika Kusini


Wengi wa waliofukiwa wanaaminika kuwa wajenzi
Watu wawili wamefariki na wengine takriban watu 50 kukwama kwenye vifusi baada ya paa ya jumba la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.
Inaarifiwa watu 29 wameweza kuokolewa.
“Shughuli hii itachukua mda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale
waliokwama,” alisema msemaji wa kampuni hiyo.Madaktari kutoka kampuni ya kibinafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban.
Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.
Inaarifiwa watu wengine 26 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majereha mabaya.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname