Leo hii rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria msiba wa Balozi Abrahamu
Sepetu (Baba mzazi wa Wema Sepetu) uliotokea hapo juzi jijini Dar es
Salaam.
Mheshimiwa kiwete amefika msibani
akiongozana na mkewe hapo kutoa pole kwa
familia hiyo kwa kuondokewa na
Balozi Sepetu ambaye hapo alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye
serikali nchini ikiwemo ya kuwa waziri wa mambo ya nje kwenye miaka ya
sabini (70) kabla ya kuwa balozi wa urusi kwenye kipindi cha miaka ya
80. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
No comments:
Post a Comment