17 October 2013

HAYA SASA WADADA..!! DAWA YA KUMKATAA MWANAUME ANAEKUSUMBUA KILA SIKU KUKUTAKA WAKATI WEWE HUMTAKI HATA CHEMBE..!!




Unaweza kukuta mwanaume anakutongoza na anakufatilia kila siku, mara akuletee zawadi kadi za upendo, mara akuletee maua ofisini, mara akuombe mtoko mara kwa mara, ili mradi keroooo kerooo na mwenyewe wala hum-feel kihivyo, lakini yeye yumo tu kila siku kujipendekeza kupita kiasi.

Hapa nitawapa mbinu ya kumkatisha tamaa mpaka mwenyewe ataachia ngazi bile kupenda


Akikuomba mtoko mkubalie lakini mpe siku siku kadhaa za kusubiri, lakini baada ya hapo uwe unampigia simu mara kwa mara kumpigisha stori zisizo na kichwa wala miguu, yaani ule muda unaodhani yuko bize ndio unampigia simu na kumsimulia stori za jinga jinga, mfano kama unaweza kumsimulia jinsi ulivyomudu kumuuwa mende aliyeingia kabatini au jinsi ulivyokuwa binti mtundu wakati ulipokuwa unasoma, ilimradi tu kumpotezea muda, akikwambia yuko bize upige baadaye, mpe muda wa dakika kadhaa kisha piga tena na stori ziwe ni hizo hizo..



Hakikisha mtoko aliokuomba hamuendi viji-mghahawa vya kijinga, tafuta mahali ambapo utamchuna achunike, chagua mghahawa aghali na pasua kichwa kumkomesha dizaini ya kumkomile nyani giladi. Kuwa makini wanaume ni wajanja sana, anaweza kujifanya anachagua mahali pengine ambapo kuna unafuu na kupasifia sana. Usikubali, mwambie wazi kwamba hapo ndipo unapopapenda na ndipo unapokwendaga siku ukitaka kujipa raha mwenyewe, akisema hana uwezo wa kumudu gharama za huo mghahawa, mwambie kama angekuwa anakupenda, basi angefanya kila namna ili aweze kukupeleka katika huo mghahawa, na kama ameshindwa, basi atakuwa hana viwango vya kuwa na mwanamke kama wewe aende kutafuta saizi zake huko Kilongawima.

Kama akikubali sio mkifika hapo unaagiza chakula cha bei ndogo. No way, hakikisha hapo ni mwendo wa Lobster, na wakati unasubiri unashtua na Famous Grouse Whisky baadaye unaagiza wine iliyokwenda shule. Bili ikiletwa mezani wewe ndio kwanza unachokonoa meno taratiibu.


Lakini pia ukimkubalia mtoko kabla ya siku ya mtoko kufika, mpigie simu umweleze kwamba unaomba mkopo wa milioni tano ili uongezee kwani umeanzisha duka la Boutique lakini fedha zimeisha kabla ya mradi kukamilika. Muahidi uamrudishia baada ya miezi mitatu, halafu msikilizie kama atakujibu nini.



Kingine, pamoja na kumkubalia kutoka naye, lakini mpe masharti ya kubadilisha muonekano wake, bila kusahau mavazi. hakikisha unamwambia anunue mavazi ya gharama, unaweza kumtajia na duka la kununua, anyoe ndevu zake vizuri pamoja na nywele. Pia akakarabati uso wake saloon kwa kufanya scrub ili apendeze. mwambie akitimiza hayo uatoka naye tena ili kukuhakikishia mwambie akutumie picha alizoppiga baada ya kujifanyia hayo mabadiliko. kama ni mtu anayejiweka katika utanashati basi wewe mshauri kitu tofauti, unaweza kumwambia awe anavaa kama sharobaro ili mradi kumbadilisha tofauti na muonekano wake


mwambie katika huo mtoko utakuja na baba yako au mjomba wako. Kama akikubali okota zee lolote la uswazi nenda nalo



Mwambie pia kwamba umeokoka na uko bikra na unampenda sana yesu kiasi kwmaba unatembea na biblia kila uendapo.




Mwambie pia kwamba hutaweza kutoka naye mpaka pale utakapomaliza matibabu ya kuacha madawa ya kulevya, kwani unahudhuria darasa katika kituo cha ushauri nasaha.


Msimulie ujinga wote uliokuwa ukifanya na bwana uliyeachana naye siku chache zilizopita, hakikisha unamsimulia mpaka yale ya kitandani ya uongo na ukweli...


Mwambie pia kwamba ni kawaida yako kabla ya kumkubalia mwanaume kwa mtoko lazima mkapime VVU..

Huyo kama hatatoka baruti basi atakuwa ni Asprin au Bujibuji

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname