Askari
wa polisi mjini Singida akiwaelekeza washitakiwa wanne wa kesi ya
unyang’anyi wa kutumia silaha kuingia kwenye gari tayari kwenda kuanza
kutumikia adhabu zao kila mmoja miaka 30 jela baada ya kutiwa hatia kwa
kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.Washitakiwa hao walitiwa hatiani
kwa kosa la kuteka gari la chuo kikuu cha SUA SU 37012 na kisha kuwapora
abiria shilingi 8.7 milioni.Pia walibomoa na kusachi jeneza lililokuwa
limehifadhiwa mwili wa marehemu mwanafunzi wa SUA,Munchari Lyoba
uliokuwa ukipelekwa mkoa wa Mara kwa mazishi.
Mshitakiwa
aliyetiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutimia silaha na kupora
abiria wa gari la SUA shilingi 8.7 milioni Hamisi Issah (wa kwanza
kulia) akipanda gari tayari kwenda kuanza kutumikia adhabu yake jela
miaka 30.Pia mwenye kofia ya bakharasia,Abubakari Jumanne naye katiwa
hatiani kwa kosa la unyang’anyi.
Washitakiwa
wanne waliotiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha
wakiwa kwenye gari la polisi tayari kwenda kuanza adahabu zao za kila
moja miaka 30.Washitakiwa hao walitiwa hatiani kwa kosa la kuteka gari
la chuo kikuu cha SUA na kupora abiria shilingi 8.7 milioni.Washitakiwa
hao pia inadaiwa walibomoa jeneza lililokuwa limebeba mwili wa
mwanafunzi wa SUA Munchari Lyoba na kulisachi kwa imani kuwa limetumika
kuhifadhi mali.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
Mahakama
ya wilaya ya Singida imewahukumu vijana wakulima wanne wakazi wa
Manispaa ya Singida adhabu ya kutumikia jumla ya miaka 120 jela baada ya
kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa shilingi 8.7 milioni kwa kutumia
silaha.
Washitakiwa
hao kabla na baada ya unyang’anyi huo walitumia silaha aina ya
bunduki,nondo,mawe na fimbo katika kufanikisha azma yao hiyo.
Washitakiwa
hao vijana ambao kila mmoja atatumikia jela miaka 30,ni Hamisi Ally
(23),Hamisi Issa (33),Khalid Hamisi (21) na Abubakari Jumanne (26) wote
wakazi wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida.
Mshitakiwa
aliyekuwa wa kwanza kwenye kesi hiyo Idd Omari (38) mkazi wa kijiji cha
Kisaki aliachiwa huru awali baada ya kutokutambuliwa na walalamikaji
katika paredi mbili za utambuzi zilizofanywa na Jeshi la Polisi.
Washitakiwa
hao pia wanadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kupora mali na fedha taslimu
waliweza kubomoa jeneza lililokuwa lina mwili wa mwanafunzi wa SUA,
Munchari Lyoba na kuchana chana sada kwa imani kwamba kuna mali
iliyokuwa imehifadhiwa humo Mwili wa Lyoba alikuwa ukipelekwa Tarime
mkoani Mara kuzikwa.
Kabla ya
kutolewa kwa hukumu hiyo,Mwendesha Mashitaka Sajenti wa Polisi,Godwel
Lawrence amesema pamoja na washitakiwa wote kutokuwa na rekodi yoyote ya
makosa ya jinai lakini kitendo walichokifanya ni cha kinyama na cha
aibu mbele ya macho ya jamii.
“Kwa
hiyo,Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama yako tukufu iwape washitakiwa
wote adhabu kali ambayo itakuwa fundisho kwao na watu wengine
wanaotarajiwa kufanya makosa ya jinai kwa kutumia silaha au nguvu ya
aina yoyote”,amesema Lawrence.
Kwa
upande wao washitakiwa kila mmoja kwa nafasi yake walitoa maombolezo
yaliyofafana kwamba wana familia zinazowatengea kwa asilimia kubwa na
kwamba kosa hilo ni la kwanza kutenda toka wazaliwe Hivyo wakaiomba
mahakama hiyo iwape adhabu nafuu.
Akisoma
hukumu hiyo iliyochukua saa moja na dakika 45,Hakimu Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya ya Singida,Flora Ndale amesema usahidi wa upande wa
mashitaka umethibitisha bila kuacha chembe chembe ya shaka kwamba
washitakiwa wana hatia kama walivyoshitakiwa.
“Walalamikaji
wote ambao walikuwa abiria kwenye gari lililokuwa likisafirisaha mwili
wa marehemu mwanafunzi wa SUA maelezo yao yanafafana wote waliweza
kuwatambua vema washitakiwa kwa msaada wa taa za gari na
mbalamwezi”,amesema.
Ndale
amesema kiongozi wa msafara huo Makaranga Nona,aliiambia mahakama kwamba
mshitakiwa wa pili na wa tatu walimwamuru kufungua ‘brief case’ mbele
ya gari huku mwanga wa taa za gari ukiwamulika.
“Kama
hiyo haitoshi,dereva wa gari hilo Kalistus Malipula ameiambia mahakama
hii kwamba mshitakiwa wane alimbebeleza kwa muda mrefu ampe simu mbili
za marehemu na maombi hayo alikuwa akiyatoa huku mwanga wa taa za gari
ukimmulika”.
Kwa
mujibu wa Mwendesha Mashitaka Lawrence washitakiwa hao wametenda kosa
hilo Desemba sita mwaka jana saa saba usiku huko katika barabara kuu ya
Dodoma – Singida eneo la kijiji cha Kisaki.
CREDIT : MO DEWJI
No comments:
Post a Comment