Mpendwa
msomaji wa JUKWAA LA WAKUBWA, Maada yetu ya leo ni mbinu za
kupanga jinsia ya mtoto wa kuzaa kabla mkeo hajashika mimba....
Siku
hizi ulimwengu umeendelea sana, matatizo mengi yanatibika kwa
msaada wa wataalamu...Hakuna tena haja ya kupigana na kupeana
talaka kisa jinsia ya mtoto...
Somo
letu ni lefu sana, hivyo tunaomba uwe mvumilivu.Kutokana na
utefu wa somo hili, tutaandika sehemu fupi katika mtandao huu
na sehemu nyingie itawekwa katika JUKWAA LA WAKUBWA ambako
kutakuwa na majadiliano ya wazi miongoni mwa wasomaji wetu....
Aidha, somo la leo litajikita zaidi katika mbinu za kuzaa mtoto wa kike.
Ni vipi jinsia ya mtoto huainishwa?
Kinyume
na wengi wanavyofikiria kwamba mwanamke au mwili wa mwanamke ndio wenye
jukumu la kuainisha jinsia ya mtoto kwa kuwa yeye ndiye anayebeba
mimba, uhakika wa mambo ni kuwa mwanamume ndie mwenye uwezo wa
kuainisha jinsia.
Kila yai la mwanamke lina chromozu mbili za X. Iwapo
manii ya mwanamume au spemu (ambayo in chromozomu X na Y) itakuwa na X
na kurutubisha yai la mwanamke lenye X tupu, basi mtoto atakayezaliwa
atakuwa mwanamke.
Vilevile iwapo spemu ya mwanaume itakuwa na Y na
kurutubisha yai la mwanamke lenye X, basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanamume.
Hivyo kwa kufahamu suala hilo, ni matumaini yetu kuwa vile visa vya
kinamama kuachwa eti kwa kuwa hawakuzaa watoto wa kiume au wa kike
vitapungua katika jamii zetu. Mke wako asipozaa mtoto wa jinsia
uitakayo, usifikiri kuwa yeye ndio mwenye makosa.
Wakati mwanamume
anapomwaga shahawa, spemu kati ya milioni 200 hadi 400 humwagwa katika
uke wa mwanamke. Baadhi ya spemu hizo huwa zina chromozomu X na baadhi
zina chromozomu Y.
Hata hivyo, ni spemu moja tu ambayo hutakiwa kwa
ajili ya kurutubisha yai la mwanamke na kuunda mimba.
Nadharia
mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kuchagua ni jinsia gani
unaitaka awe nayo mwanao, zinategemea suala la kuandaa mazingira katika
uke na mwili wa mwanamume na mwanamke, yatakayosaidia spemu ya baba
yenye chromozomu inayotakiwa irutubishe yai la mama, na hivyo kutungwa
mimba ya jinsia inayotakiwa.
Njia ya Dr. Shettles ya kuzaa mtoto wa kike
Njia
hii imekuwa ikitumiwa na watu wengi kwa miaka mingi sana na imewasaidia
kuweza kuzaa mtoto wa kike.
Wengi wanasema kuwa uwezekano wa kufanikiwa
njia hii ni asilimia 90. Njia ya Dr. Shettles inategemea msingi kwamba,
chromozomu Y (yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kiume) ni
ndogo na yenye kwenda kwa kasi zaidi ikilinganishwa na chromozomu X
(yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kike) ambayo ni kubwa na
huenda polepole.
Pia kwa kutegemea kuwa chromozomu X inaishi muda
mrefu zaidi kuliko ile ya Y. Hivyo Dr. Shettles anashauri kuwa iwapo
unataka kuzaa mtoto wa kike uhakikishe kuwa:
No comments:
Post a Comment