FAMILIA ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’
inadaiwa kumwachia Mungu ishu ya binti huyo kukamatwa na madawa ya
kulevya Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa ndugu
mmoja wa familia hiyo aliyeomba jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia
Mungu ishu hiyo kwani ndiye anayejua ukweli.
“Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald Waya) ni mlokole, sasa
amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo hayuko tayari
kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida,” alisema ndugu huyo.
Habari
zinazidi kudai kwamba, mzee huyo aliwahi kuchukizwa na kitendo cha
binti yake huyo kujiingiza kwenye sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye
muziki.
Hilo liliwahi kubainishwa na Masogange mwenyewe miaka ya nyuma
alipohojiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kupitia safu ya Ten
Questions (Maswali Kumi) ambapo ilikuwa hivi:
TQ: Inasemekana
umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, walokole, wao
wanachukuliaje suala la wewe kuingia kwenye mambo ya kuuza sura tena
wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?
Agnes: Mh! Baba yangu hataki kabisa kusikia mambo ya muziki na
niliwahi kukosana naye lakini nalazimisha kwa kuwa ni moja ya ajira.
Jitihada za kumpata baba wa Masogange ziligonga mwamba baada ya namba iliyotolewa na ndugu huyo kutokuwa hewani.
Masogange
na nduguye, Mellisa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakiwa na ‘unga’ kilo 150 aina
ya crystal methamphetamine wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

No comments:
Post a Comment