Taarifa
iliyotufikia inaeleza kuwa yule Dereva
aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2492 CPL-Elikiza na
kutokomea, amekamatwa jana usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa
askari huyo maeneo ya Bamaga mapema juzi mchana.
kwa
Mujibu wa kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani
nchini,Kamanda Mohamed Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye
ajali hiyo limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini
Dar.
Kamanda
Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani
kwa Marehemu,hukoUnunio,kaskazaini mwa jiji la Dar. Rais Kikwete alifika
kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha Mume na watoto
watatu.
No comments:
Post a Comment