20 March 2013

NANCY SUMARI AZINDUA KITABU CHA WATOTO NYOTA YAKO


Miss World Africa 2005, Nancy Sumari leo amezindua kitabu chake cha watoto kiitwacho Nyota Yako. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwemo mamiss Tanzania wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe na Faraja Nyalandu.
Nancy Sumari akizungumza kwenye uzinduzi huoNancy Sumari akizungumza kwenye uzinduzi huo
Wengine ni pamoja DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya watoto na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Profesa Esther Mwaikambo, Jokate Mwegelo, Shaa, Ally Remtullah. Fina Mango na wanafunzi mbalimbali.

Akizungumzia jambo lililomsukuma kuandi ka kitabu hicho, Nancy alisema:
Vilinisukuma vitu vingi, kwanza nafasi ya mwanamke kwenye jamii yetu, umuhimu wake, sababu ya kumuenzi na kumsherehekea na kutambua michango yetu, mwanamke mdogo, msichana mdogo, mama zetu, bibi zetu. Kuna kila sababu ya sisi kuangaliana na kutambuana na pia kufananisha.
IMG_7259
Profesa Mwaikambo akikielezea kitabu hichoProfesa Mwaikambo akikielezea kitabu hicho
Profesa Mwaikambo akimuonesha picha ya kwenye kitabu hicho mtoto wa Nancy, ZuriProfesa Mwaikambo akimuonesha picha ya kwenye kitabu hicho mtoto wa Nancy, Zuri
Sababu baada ya kutembea kwenye shule nyingi na kuzungumza na wasichana wengi nimegundua kwamba story zetu zinafanana. Changamoto ni nyingi tunazozipitia na tunafanana kwa vitu vingi kwahiyo nikaona ni vyema nikawafananisha wasichana wengi wakamwangalia mwanamke kama Dokta Migiro wakasikiliza story yake, wakajiona kwenye hiyo hadithi, wakaona uwezo wao wa kufikia alipofikia Dokta Migiro.
K-Lyinn akisaini kitabu cha waliohudhuria uzinduzi huoK-Lyinn akisaini kitabu cha waliohudhuria uzinduzi huo
MC wa uzinduzi huo Rebeca GyumiMC wa uzinduzi huo Rebeca Gyumi
Ally RemtullahAlly Remtullah
K-Lyinn akifuatilia kwa ukaribu uzinduziK-Lyinn akifuatilia kwa ukaribu uzinduzi
Faraja NyalanduFaraja Nyalandu
Nancy aliongeza kuwa mwanae pia alimchochea kuandika kitabu hicho. 
“Baada ya mimi kuwa na Zuri nikaona kuna umuhimu wa yeye kuangalia wanawake wa kitanzania kama role models. Anaweza akawaangalia wanaojulikana akawajua pia lakini kuna kila sababu ya kuangalia wanawake wengi na michango mingi inayofanyika kwenye jamii yake akawatambua wanawake na kuwaenzi.”
Kuhusu upatikanaji wa kitabu hicho, anasema, “kwanza nitakisambaza kwenye shule za msingi bure, halafu nitakisambaza kwenye bookshop ambako kitauzwa, kwahiyo watoto wa shule ya msingi watakuwa na access nacho bure lakini wengine wengi watakinunua kwenye bookshop. Hizo hela ambazo zitapatikana zitaprint kitabu na kukisambaza mbali zaidi.” 
“Nimepata mchango mkubwa sana kutoka Bongo5 Media Group ambao wamenisaidia kufanikisha kitabu hiki, nawashukuru sana,” alisema Nancy.
Farja Nyalandu akizungumzaFarja Nyalandu akizungumza
IMG_7200
IMG_7201
K-Lyinn akizungumza na Ally RemtullahK-Lyinn akizungumza na Ally Remtullah
K-LyinnK-Lyinn
Kaka yake Nancy Sumari, Davis Abraham Sumari (kulia)Kaka yake Nancy Sumari, Davis Abraham Sumari (kulia)
Fina MangoFina Mango
IMG_7211
IMG_7213
Fina Mangi na Faraja NyalanduFina Mangi na Faraja Nyalandu
Akizungumzia kasumba ya watanzania wengi kutopenda kusoma vitabu na jinsi alivyokabiliana nayo Nancy anasema, “nilimshirikisha mchoraji mzuri sana kwasababu nilitaka kumvutia mtu kwa wepesi kwanza kiwe kifupi, yaani kidogo. Ni kitabu ambacho unaweza kukipitia ndani ya dakika tano. Kuna picha nyingi lakini meseji yake ni nzito sana.”
Kwa upande wake Profesa Mwaikambo(74), ambaye mwaka huu ubalozi wa Marekani ulimtunuku tuzo ya haki ya Dk Martin Luther King amempongeza Nancy kwa kuandika kitabu hicho na kusema kuwa watoto wengi hasa wenye kuanzia umri wa miaka mitatu wataweza kukifurahiia kwa kuangalia picha tu.
Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari King'ongo ya Kimara jijini Dar es Salaam Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari King’ongo ya Kimara jijini Dar es Salaam
Shaa na Nancy wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunziShaa na Nancy wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi
Picha ya pamoja na Nancy, K-Lyinn, Ally Remtullah na rafikiPicha ya pamoja na Nancy, K-Lyinn, Ally Remtullah na rafiki
IMG_7238
IMG_7240
Nancy na FarajaNancy na Faraja
Mamiss Tanzania wa zamani wakiwa wameshikilia kitabu hichoMamiss Tanzania wa zamani wakiwa wameshikilia kitabu hicho
Mwanafunzi akifurahia kumsomea mzungu kilichoandikwa kwenye Nyota YakoMwanafunzi akifurahia kumsomea mzungu kilichoandikwa kwenye Nyota Yako
Alisema ubongo wa mtoto huanza kukua akiwa na umri wa miezi tisa na akifikia mwaka mmoja unaweza kumfundisha chochote na akaelewa.
“Hakuna mtoto mdogo mjinga, hakuna, labda kama amezaliwa na mtindio wa ubongo, lakini mtoto yeyote anayezaliwa na mwanamke ana akili za kutosha kabisa lakini lazima awe exposed “alisema Profesa Mwaikambo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname