Moshi mweusi ulifuka jana jioni kutoka kwenye dohani
huko Vatican ikiwa ni ishara kwamba Baraza la siri la Makadinali bado
halijampata Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki baada ya kupiga kura ya
kwanza.
Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana ambapo
Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa faragha ili kumchagua
atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu
mwishoni mwa mwezi uliopita.
Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.
Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.