1. Jokate Mwegelo
Mrembo huyu anafahamika pia kwa jina la Kidoti – jina ambalo
limeanzisha kampuni yake ya fashion yenye jina hilo. Ni mshiriki wa Miss
Tanzania, mbunifu wa mitindo, mtangazaji na msanii pia wa muziki.
Hajawahi kutoa wimbo wake mwenyewe zaidi ya kushirikishwa tu. Alianza
kusikika kwenye ngoma ya AY King and Queens. Mwaka jana alishirikishwa
kwenye albam ya Kala Jeremiah, Pasaka na pia mwaka huu amesikika kwenye
ngoma ya Lucci ‘Waters Up’ Kuna project zake kadhaa pia kwenye studio za
TransformaX ambazo hazijatoka.
2. Nuru the Light
Nuru Magram aka Nuru the Light ni blogger na mwanamuziki aishie
Stockholm, Sweden. Pamoja na kupenda fashion, Nuru amekuwa akirudi
Tanzania na kutengeneza ngoma kadhaa zikiwemo ‘Muhogo Andazi’
aliomshirikisha Bob Junior, Chapa Lapa na zingine.
3. Feza Kessy
Feza Kessy ni msanii mpya aliye chini ya usimamizi wa kampuni ya AY,
Unity Entertaiment. Mwezi uliopita aliachia single yake ya kwanza
iitwayo Amani ya Moyo na ambayo inafanya vizuri kwa sasa. Tangu aachie
wimbo wake wa kwanza, mrembo huyu aliyewahi kushikilia taji la Miss Dar
City Centre amewathibitishia watanzania kuwa si kwamba kabarikiwa uzuri
tu bali pia sauti tamu ya kuimba.
4. Zuhura
Zuhuru Mrisho si msanii maarufu sana nchini licha ya kuwepo kwa muda
sasa. Aliwahi kushika taji la Nokia Face of Africa 2006, lililomjumuisha
kwenye ramani za mastaa wa Bongo. Mrembo huyo aliyepitia nyumba ya
vipaji ya THT, alitambulishwa kwenye game ya muziki kupitia wimbo wenye
jina la Limupenzi, na Shida na Raha aliyompa shavu Banana na mpaka sasa
ana albam moja. Kwa sasa ana video mpya ya wimbo wake Songesha.
5. Menynah Atick
Menynah ni mshiriki wa shindano la Bongo Star Search mwaka jana na
ambaye aliingia kwenye shindano hilo kwa usaili wa njia ya simu. Ni
msichana mdogo ambaye baada ya shindano hilo kumalizika ameachia wimbo
uitwao ‘Dream Tonight’. Pia yeye na wenzake wawili wameanzisha kundi la
muziki lililo chini ya producer Lamar, Shostiz.
6. Linah
Nani asiyemfahamu Linah? Ni miongoni mwa wasanii wa kike wenye sauti
tamu kuwahi kutokea Tanzania. Pamoja na Mungu kumpa sauti, amempa pia
urembo unaowadatisha wanaume wengi.
7. Baby J
Baby Jay ni msanii kutoka Zanzibar ambaye mara nyingi amekuwa karibu
na kundi la Offside Trick. Macho yake huwachanganya wanaume wengi.
8. Shaa
Sarah Kaisi aka Shaa ni mrembo mwenye historia ya kufanya hits tu.
Tangu ashiriki shindano la kusaka vipaji la East Africa Coca Cola Pop
stars, hajawahi kusimama kwa kuachia ngoma kama Shoga, Siri ya Penzi na
sasa akiwa na hit mpya, Promise.
9. Shilole
Shilole anafahamika kama malkia wa mduara kwa sasa na amekuwa kivutio
kikubwa kwenye jukwaa kila anapotumbuiza kwa jinsia anavyojua kucheza
na kiuno chake. Ameshatoa hits kibao zikiwemo Lawama, Viuno Tucheze na
Dudu.
10. Vanessa Mdee
Vanessa Mdee ni mrembo mwingine aliyeweka historia mwaka huu kwa
kutoa single iliyoingia kwenye top ten ya nyimbo zilizopakuliwa zaidi
(downloaded) mtandaoni, Closer. Pamoja na kuupata umaarufu kutokana na
kazi yake ya utangazaji, mwaka huu amejipatia sifa kede kede kwa
kuonyesha uwezo mkubwa katika kuimba.
11. Recho
Recho ni msanii wa THT ambaye kabla ya kugundua kuwa ana uwezo mkubwa
kuimba alijiona kuwa ni muigizaji wa filamu zaidi. Mpaka sasa ana
nyimbo tatu tu, Upepo, Kizunguzungu na Nashukuru Umerudi lakini kila
shabiki wa muziki wa Bongo analijua jina lake.