Hivi ndivyo Usomekavyo Ubao wa Matokeo katika Uwanja huu wa Taifa jijini na TIMU
ya soka ya Taifa, Taifa Stars jioni hii imewachapa mabingwa wa Afrika,
Zambia bao 1-0 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya soka iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya
Zambia katika mchezo wa kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda goli 1-0.
Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
Mchezaji
wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya
Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
Mchezaji
wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijaribu kutaka kumtoka beki wa
Taifa stars,Salum Aboubakar wakati wa Mchezo wa Kirafiki unaoendelea
hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Taifa stars wanaongoza kwa
bao moja lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachari,Mrisho Ngassa
mnamo dakika ya 45 ya mchezo.
Shujaa
wa Taifa Stars katika mechi hiyo alikuwa mshambuliaji Mrisho Ngasa
aliyefunga bao hilo la pekee na la ushindi katika kipindi cha kwanza.Ngasa alifunga bao hilo kwa shuti kali akiwa pembeni ya uwanja, ambalo liligonga mwamba wa juu wa goli na kutinga wavuni.
Katika mechi hiyo, mchezaji aliyeng'ara kwa upande wa Taifa Stars alikuwa kiungo
Mbali na Sure Boy, kiungo mwingine Frank Domayo naye alicheza vyema nafasi ya kiungo mshambuliaji, akishirikiana vyema na Mwinyi Kazimoto na Ngasa, ambao walikuwa mwiba kwa mabeki wa Zambia.
Amri Kiemba alilazimika kucheza mechi hiyo akiwa majeruhi, lakini aliweza kuelewana vyema na wenzake japokuwa hakuwa na kasi iliyozoeleka. Taifa Stars ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Zambia ilikianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko ya wachezaji watano kwa mpigo kabla ya kuongeza wengine wawili kadri dakika zilivyokuwa zikiyoyoma. Walipotaka kuingiza wachezaji wengine wawili, mwamuzi Kirwa kutoka Kenya aliwakatalia.
Katika kipindi hicho cha pili, Taifa Stars ilimpumzisha Khamis Mcha na kumwingiza Simon Msuva kabla ya baadaye kuwatoa Ngasa na beki Kevin Yondan na kuwaingiza Amir Maftah na Nadir Haroub Cannavaro.
Wakizungumza wakati wa mchezo huo, baadhi ya mashabiki walimpongeza kocha Kim Poulsen kwa uamuzi wake wa kuwachezesha wachezaji vijana wengi na wasiokuwa na majina.
Mshambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ambao wamekuwa wakidengua kuja kuichezea Taifa Stars, walijikuta wakiwa kwenye wakati mgumu baada ya kuzomewa na mashabiki.
Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Mrisho Ngasa/Amir Maftah, Mwinyi Kazimoto, Khamis Mcha/ Simon Msuva
Zambia- Danny Munyao, Chintui Kapamba,Hichani Himonde,Chisamba Lungu,Jame Chamanga/Shadrack Malambo,
Christopher Katondo/Stoppila Sunzu,Felix Katongo,Nathan Sinkala/Evans
Kangwa,Roderick Kabwe/Francis Kasonde na Issac Chansa.




