31 October 2012

SHINDANO LA UNIQUE MODEL 2012 LAZINDULIWA



Mkurugenzi wa shindano hayo, Methuselah Magese akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).

SHINDANO la kusaka wanamitindo wenye vegezo vya kipekee nchini, linaloratibiwa na kampuni ya Unique Entertainment, leo limezinduliwa rasmi katika hoteli ya Holiday Inn Posta jijini Dar es Salaam.


Magese (katikati) akiwa pamoja na bodi yake ya uandaaji…
 
Shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania(unique model) linaloandaliwa na Unique Entertainment
limezinduliwa leo jumatano kwa kishindo katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo katika ya jiji la Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari hao katika ufunguzi huo mkurugenzi wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa mchakato wa shindano umefunguliwa rasmi ili kutoa fursa ya wadhamini kujitokeza kwa wingi kudhamini shindano hilo ambalo litakuwa na mvuto wa aina yake kwa msimu huu wa pili.

Pia wanamitindo wenye sifa za kimataifa wameombwa kujitokeza kwa wingi katika usaili utakaofanyika tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada Apartments.

Tumeboresha shindano kwa kiwango cha hali ya juu tofauti na ilivyokuwa hapo awali,lengo ni kulifanya shndano hili liwe la heshima,hadhi na linalotimiza lengo lake la kuvumbua na kuinua vipaji vya wanamitindo wa kchipikizi.

“Tunaomba wabunifu wadogo kwa wakubwa wajitokeze kuja kuonyesha umahili wao katika shindano hili ambapo mwaka huu tutakutanisha wabunifu wengi wa mavazi nchini Tanzania katika shindano moja kwa lengo la kuwainua wabunifu wadogo na kuendelea kuwatangaza wabunifu wenye majina makubwa katika tasnia ya mitindo hasa katika kipindi hiki maridhawa cha mwisho wa mwaka” alisisitiza Magese.

Katika msimu huu wa pili wa unique model kutakuwa na nyongeza ya mataji mengine madogo matatu amabayo ni “model photogenic 2012”,”model talent 2012” na “model with good manner 2012” ambapo mataji hayo yatakuwa chini ya taji kuu la “Unique model of a year 2012”.

Fainali za shindano la Unique model 2012 zitafanyika mwishoni mwa mwezi Desemba ambapo kamati ya maandalizi imedhamilia kufanya onyesho lenye hadhi kuanzia ubora wa washiriki wenye vigezo vya uanamitindo ambao wataleta mabadiliko katika tasnia ya mitindo nchini.

Shindano la Unique model lilianzishwa mwaka 2010 ambapo kwa mwaka huu ni mara ya pili kufanyika,Asia Dachi ndiye mwanamitindo anaeshikilia taji hilo mpaka sasa.

Wito umetolewa kwa makampuni kujitokeza kuchukua mabalozi ambao ni wanamitindo washiriki kwa lengo la kufanya nao kazi za kutangaza bidhaa ama huduma inayotolewa na kampuni husika kwa lengo la kutoa ajira kwa wanamitindo hao wanaochipukia katika tasnia.

Unique model 2012 imedhaminiwa na Dtv,Gazeti la Tanzania Daima,Mashujaa investment ltd,Sophernner Investment co ltd,K.d.surelia,young don records,Kiu investment ltd,Oriental bureau de change,100.5 Times fm,J’s professional ltd,Lamada apartments hotel, na Unique entertainment blog.

Comments system

Disqus Shortname