Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola |
Mbunge
wa Mwibara Kangi Lugola kupitia CCM bungeni july 17 2012 amesema
polisi wamtafute Fadhili Kweka mwenye mtandao wa uhalifu ndani ya jeshi
la polisi.
Amesema
“kuna mtandao mkubwa wa uhalifu ndani ya jeshi la polisi na ushahidi
ninao, wanatoa kwa wahalifu taarifa za wananchi wanaomiliki silaha ili
wahalifu wajue wananchi wana uwezo kiasi gani wa kujihami ili waende
kufanya uhalifu, IGP unaenisikiliza naomba anza na mtumishi wenu
anaitwa Fadhili Kweka anaomtandao wa uhalifu ndani ya jeshi la polisi,
hainiingii akilini anapata wapi taarifa za wananchi wanaomiliki silaha
alafu anawapa wahalifu, anzeni na huyo na nitawapa ushahidi wa kutosha”
Hiyo
ndio kauli ya Mbunge Kangi Lugola ambae alikua akitoa hiyo mistari
wakati wa kuchangia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi….
unaweza kumsikiliza zaidi hapo chini ufahamu yote aliyosema….
safi sn 2nataka wabunge wa namna hii wanaojitoa mhanga na kuweka mambo hadhalani.
ReplyDelete