16 July 2012

GARI la KWANZA KUSAJILIWA kwa JINA BADALA YA NAMBA HILI HAPA.

 Kuanzia mwaka mpya wa fedha (2012-2013) Mamlaka ya Mapato Tanzania imeanza kusajili magari kwa kutumia majina ikiwa ni nyongeza ya kutumia namba kama ilivyokuwa imezoeleka na wengi. Pichani juu na chini ni gari la kwanza kupewa usajili huo wa kutumia jina la mmiliki wake.


5 comments:

  1. Inaniuma wengine hatuna hata ela ya kula mwingine anafanya hayo

    ReplyDelete
  2. Hiyo ni kufuru jamani ,kwa nini asiwasaidie hata maskini wanaoteseka hata huko kijijini kwao moshi.Ni haki yake kujitanua,lakini angetumia busara na ukarimu wa kuwasaidia wengine ingempa heri kuliko kutengeneza gari hilo kwa milioni 50 ambazo angenunua gari lingine,na labda angejengea nyumba watu maskini huko vijijini.Ila masikio na macho yangu mbona hayaamini kama kuna binadamu wa namna hiyo hapa Tanzania ambaye anaweza kununua gari la kiasi hicho cha pesa alitumie hapo Tanzania wakati wengine wanakosa hata mlo mmoja tu wa mchana au usiku.

    ReplyDelete
  3. Kama nakumbuka vizuri kusajili gari kwa jina lako ni milioni tano na sio 50 wadau!

    ReplyDelete
  4. Halafu inaweza ikawa siyo kufuru na hujui kama huwa anawasaidia watoto ama laHH?!!ila usahihi wa kusema hiyo ni gari ya kwanza pia yaweza isiwe kweli kwani kwa mfano kama DELINA ana magari 6 na akataka yote yatumie DELINA ina maana atakuwa na DELINA 1 hadi DELINA 6 so tupatieni uhalisia wa kusema ni gari ya kwanza jamani.

    ReplyDelete
  5. Sio kwei unaposema ni gari ya kwanza, maybe iwe ni gari ya kwanza machoni kwako kuiona but zipo kibao kwa sasa.
    ikiwemo gari la baba mkwe ambapo yeye kasajili "BOSCCO"
    from Kilimanjaro.

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname